Search This Blog

Friday, January 25, 2013

Mapigano makubwa yazuka Moro, Mtwara

• Polisi, wananchi watwangana

MAPIGANO makubwa yamezuka katika mikoa ya Morogoro na Mtwara kiasi cha kusababisha kifo cha mtu mmoja, Mohamed Msigala (60), na kuharibiwa kwa magari na mali nyingine ikiwemo kuchomwa moto kwa mahakama ya mwanzo.

Mapigano yaliyozuka mkoani Morogoro yamehusisha wakulima wa vijiji vya Msolu, Mbigili, Mambengwa na Mabwegere vilivyoko kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro, yakiwaacha mamia ya wanawake na watoto wakiyakimbia makazi yao kwa hofu ya kuuawa.

Mapigano hayo yametokea kati ya wakulima na wafugaji wa vijiji hivyo wanaogombea ardhi, inayodaiwa kuuzwa kinyemele kwa baadhi ya mawaziri waandamizi na wafugaji, huku kukiwa na tishio la kufutwa kwa baadhi ya vijiji.

Mali kadhaa yakiwemo magari yameharibiwa vibaya, ambapo nyumba tano za kulala wageni katika eneo la Dumila zimeshambuliwa, wananchi kupora mali mbalimbali zinazodaiwa kumilikiwa na wafanyabiashara wa jamii ya Kimasai.

Mapema majira ya saa 2:30 asubuhi, mamia ya wananchi hao walifanya maandamano kutoka mwanzo hadi mwisho wa mji huo na kutanda kwenye barabara, kabla ya kuiziba kwa mawe na magogo makubwa na kuchoma matairi.

Kikosi cha polisi cha kutuliza ghasia kililazimika kuingilia kati na kupambana na waandamanaji hao kwa mabomu ya machozi na virungu na kufanikiwa kuwakamata idadi kubwa ya wananchi hao.

Pamoja na barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma lakini pia wananchi hao walifunga barabara ya Dumila- Kilosa na hivyo kuyafanya magari yaliyokuwa yakitumia barabara hiyo kusimama kwa muda mrefu.

Habari zinasema kuwa vurugu hizo zimechochewa zaidi baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai kuingiza mifugo kwenye mashamba yenye mazao, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa licha ya uongozi wa kijiji hadi mkoa kufikishiwa malalamiko hayo.

Mashamba yanayolalamikiwa yako katika eneo la Mabwegere ambalo linadaiwa kuuzwa kwa baadhi ya mawaziri, na hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo alitangaza kuwa ni mali ya wafugaji jambo ambalo lilipingwa na wakulima.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera alilazimika kukatisha shughuli zake za Kibunge huko Dodoma na kurejea mkoani Morogoro kuangalia hali ilivyo.

Hata hivyo, akihojiwa kwa njia ya simu, Bendera alionekana kufura akidai kwamba kulikuwa na upotoshaji mwingi uliochangia kutoeleweka vema kwa suala hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amethibitisha kukamatwa kwa watu kadhaa katika vurugu hizo na kwamba ulinzi umeimarishwa.

Tuhuma za kuhusika kwa baadhi ya mawaziri katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, huku mmojawao akidaiwa kununua hekari 400, zilianikwa mapema mwezi jana, huku mamlaka zikiwa zinataka kufuta hati miliki ya kijiji cha Mabwegere.

Ilielezwa kuwa watu wasiojulikana waliingia kijijini hapo na kuingilia mipaka na kung’oa alama zilizowekwa na serikali licha ya kuamriwa kuwa mahakama itekeleze zoezi hilo baada ya wanakijiji hao kushinda kesi.

Mbali na kung’olewa kwa mipaka hiyo, watu kutoka maeneo mbalimbali waliendelea kuingia katika kijiji Mabwegere kinyume cha utaratibu na kufungua mashamba ambayo yanadaiwa kumaliza maeneo ya malisho ya mifugo iliyomo kijijini humo. Kijiji cha Mabwegere ni cha wafugaji ambacho ndicho kilichoathiriwa zaidi na machafuko.

Kwa mujibu wa barua yao ya malalamiko, wananchi hao walisema kuwa kwa sasa wamepoteza imani na mkuu wa wilaya na mkurugenzi wao kwani walitegemea kuwa migogoro ya ardhi iliyosababishwa na wakulima kujichukulia eneo la wafugaji ingetatuliwa kwa kuzingatia sheria na utawala bora.

Ofisa mtendaji mstaafu wa kijiji hicho, Sadiki Mwibela, alisema kuwa migogoro mikubwa imekuwa ikitokea kati ya wakulima na wafugaji.

“Kwa sasa msimu wa mvua umeanza, machafuko yanaweza kutokea, lakini mimi kwa kuwa nilikuwa nafuatilia haki za wafugaji waliokuwa wanaporwa mifugo yao kwa kuwa tulikataa kuuza eneo letu, nilifukuzwa kazi, nikakamatwa nikapelekwa jela, nilipotoka nikakuta wameweka mtendaji mwingine,” alisema.

Viongozi wengine ambao waliomba wasitajwe gazetini walisema kuwa walilazimishwa na mkuu wa wilaya kwenda ofisini na kuandika muhtasari ili waziri huyo apewe eneo.

Mtwara hakukaliki

Mkoani Mtwara wananchi wamechoma moto mahakama ya mwanzo na kuharibu gari la polisi, kufuatia kuzuka kwa mapigano kati yao jana.

Mapigano hayo yalianza baada ya askari polisi kuwavamia wananchi katika eneo la Sabasaba waliokuwa wamefurika kushuhudia watu wanaoaminika kuwa wachawi walionaswa usiku wakifanya vitendo vya kishirikina.

Mmoja wa wananchi walioshuhudia tukio hilo, amesema kuwa polisi waliokuwa ndani ya gari wakiwa na bunduki, walifika eneo hilo baada ya kupewa taarifa na msamaria mwema kuwa kulikuwa na vurugu za wananchi waliotaka kuwaua watu hao wawili waliokutwa wakifanya vitendo hivyo vya kishirikina.

Hatua hiyo ya polisi, iliwakasirisha wananchi walioamua kujibu mapigo kwa kuwashambulia kwa mawe na kisha kuharibu gari lao na kulazimika kukimbia kusalimisha maisha yao.

Habari zinasema kuwa askari polisi walirudi wakiwa katika magari matatu na ndipo walianza kuwashambulia wananchi popote walipowakuta katika eneo la soko kuu la Mtwara na kuharibu mali.

Wananchi nao waliamua kujikusanya kwa wingi na ndipo yakazuka mapambano mengine makubwa yaliyosababisha kuchomwa moto kwa mahakama hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa hakuweza kupatikana, kwa vile simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani kwa muda mrefu.

Polisi waonya

Jeshi la polisi nchini, limewataka wananchi kutii sheria bila shuruti, na wasitumie mwanya wa makosa yanayofanywa na baadhi ya askari au wananchi wengine waliovunja sheria kuhalalisha uvunjaji mwingine wa sheria, kwani makosa mawili hayafanyi haki moja.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, aliiambia Tanzania Daima Jumamosi kuwa ni jambo baya na la hatari ikiwa sasa wananchi wataamua kuchukua sheria mikononi kuvamia vituo vya polisi na kuua askari, au kuvamia mali za watu.

Senzo amelalamikia vitendo vinavyozidi kushamiri nchini kwa wananchi kuvamia vituo vya polisi, kuchoma moto vituo, au wananchi kuacha kabisa kutii amri halali za jeshi la polisi pindi askari wanapofika katika maeneo yenye fujo.

Alikiri kuwa ndani ya jeshi hilo kuna askari wachache wakorofi ambao sio waadilifu, lakini huo sio mwanya kwa wananchi kuhalalisha, kujeruhi au kuvamia vituo vya polisi.

“Tunakataza uvunjaji wa sheria iwe ni kwa askari au raia, ndio maana inapothibitika kuwa polisi amekosea, anachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za jeshi,” alisema.

Makachero wavamia vyuo

Katika hatua nyingine watu wanaoaminika kuwa makachero wa serikali, wameingia mkoani Mtwara na sasa inadaiwa wanaendesha uchunguzi wa siri wenye lengo la kuwabaini watu wanaotuhumiwa kuwa vinara wa kupinga ujenzi wa bomba la gesi.

Habari za kuaminika zimesema kuwa makachero hao walianza kuwasili mjini hapa, siku sita zilizopita na wamejizatiti katika baadhi ya taasisi nyeti vikiwemo vyuo vya elimu ya juu, kunakoaminika kuwa moto wa hamasa wa kupinga ujenzi huo umeshika kasi.

Mbali na vyuoni, makachero hao wamekuwa wakiendesha uchunguzi katika ofisi za serikali, kujua ni wafanyakazi gani wanaoshabikia jambo hilo na kwamba watakaobainika watakamatwa na kufunguliwa mashtaka mbalimbali yakiwemo ya uchochezi.

Mangula acheza rafu CHADEMA

MPANGO mchafu wa kukichafua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa umefichuka, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Philipo Mangula akituhumiwa kuratibu harakati hizo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya CCM, zimebainisha kuwa, chama hicho kimechapisha mamia ya kadi za CHADEMA ambazo zimesambazwa kwa watu maalumu walioandaliwa ambao wameambiwa wazirejeshe leo wakati wa mkutano wa hadhara na kumkabidhi Mangula, wakidai wameihama CHADEMA.

Imebainika kuwa, zaidi ya wanafunzi 200 wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa tayari wamekabidhiwa kadi hizo, na fedha za kujikimu ambapo watajitangaza kama wana-CHADEMA waliohamia CCM baada ya kuchoshwa na upinzani katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa.

Mbali na kadi, CCM pia imetengeza fulana za CHADEMA walizopewa wanafunzi hao, na kwamba chama hicho kimemwaga maelfu ya fedha kwa wasomi hao kama njia ya kufanikisha mpango huo.

Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Mtama Joseph amekiri kusikia taarifa hizo, lakini akadai kuwa kama ni kweli basi, utakuwa ni mpango unaotumika na watu waliopoteza mwelekeo.

“Ni kweli kuna taarifa hizo zimezagaa hapa chuoni kwamba kuna wanafunzi 200 ambao wamepewa sh 5,000 kila mmoja, na kadi zenye nembo ya CHADEMA ili warudishe kwenye mkutano wa CCM utakaofanyika kesho (leo) katika viwanja vya Mwembetogwa,” alisema.

Mtama alisema kama habari hizo ni za kweli, litakuwa jambo la kusikitisha na linaloonesha kuwa watu walioshindwa kufikiri na kuwajibika hutumia mbinu chafu kwa kuwa hawana fikra zingine zaidi ya rushwa.

Mmoja wa vijana wanaodaiwa kutumiwa katika mpango huo (jina limehifadhiwa) amekiri kuwa miongoni mwa viongozi wanaoratibu mpango huo na kwamba yeye na wenzake wameahidiwa sh 500,000 kila mtu pindi watakapofanikisha hujuma hiyo.

Kijana huyo aliyeomba jina lake lisitajwe kwa kuhofia usalama wake, alisema tayari kuna vijana 17 ambao wameandaliwa pamoja na kuratibu, lakini pia kufanya kazi ya kuichafua CHADEMA kwa namna watakavyoelekezwa pindi wakifika mkoani hapa kwa ajili ya mikutano ama shughuli nyingine.

Mbali na hilo, kijana huyo alisema CCM pia imeandaa magari kusomba wanachama wake kutoka vijijini kuletwa katika mkutano wa leo kwa madai ya kutaka ionekane ina wanachama wengi, hivyo kuondokana na aibu ya kukosa watu katika mkutano wake.

Katibu wa CHADEMA Manispaa ya Iringa, Suzan Mgonukulima alisema kuna mbinu chafu zilizobainika kutumika kuhujumu CHADEMA ambazo wananchi wanatakiwa kuwa nazo makini.

Alisema kufichuka kwa siri hizo, ni ishara wazi kuwa watu wanaojitangaza kurudi CCM sio wanachama halisi, bali waigizaji na kuonya kuwa mchezo huo ni ishara ya wazi kuwa sasa serikali inatishiwa na CHADEMA.

Diwani wa Kata ya Mivinjeni, Frank Nyalusi (CHADEMA) ambaye pia ni mjumbe wa kamati tendaji ya wilaya, alisema propaganda za CCM zimepitwa na wakati na kwamba ni dalili za kutapatapa kwa sababu wanajua kuwa mwaka 2015 wanaachia ngazi.

Wabunge CHADEMA waishukia serikali

Jijini Dar es Salaam, wabunge wawili wa CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) wameufananisha uongozi wa Serikali ya CCM na ule wa kifalme uliofitinika kutokana na mawaziri wake kutofautiana katika maamuzi mbalimbali ya kitaifa.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Mombasa jijini Dar es Salaam, wabunge hao walisema mawaziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, hawaelewani hali inayoweza kuifanya nchi kuwa katika hatari ya kushindwa kufanya mambo ya maendeleo kwa wakati.

Mchungaji Msigwa, alisema hivi karibuni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Stephen Wasira aliwaamuru wananchi waendelee kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Alisema katika hifadhi ya Serengeti kuna mlango unaotumiwa na wanyama na kwamba Wasira akijua sheria hairuhusu kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo lolote la uhifadhi aliwahimiza wananchi wajenge nyumba na shughuli za kilimo hadi alipoonywa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

“Wanasema CHADEMA itakufa wakati wao ndio wanaelekea kuzimu kama huyu Wasira aliyeonywa na Kagasheki juu ya kuhamasisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo la Serengeti, lakini ameendelea kupuuza na kusema ni heri afe kuliko kufuata taratibu,” alisema Msigwa.

Akizungumzia ujangili katika mkutano huo, Msigwa alisema serikali inapaswa kupanga mipango madhubuti kukabiliana na hali hiyo badala ya mawaziri wake kutumia muda mwingi kutaka kuihujumu CHADEMA.

Alisema kutokana na udhaifu huo wa Baraza la Mawaziri na hofu ya kuondolewa madarakani ifikapo 2015, wameshindwa kuunganisha nguvu ya pamoja za idara ya ulinzi na usalama hata kufikia baadhi ya watendaji kujiingiza katika matukio ya ujangili kama ilivyotokea hivi karibuni kwa askari wa Jeshi la Wananchi kukutwa akisafirisha pembe za ndovu.

Kwa upande wake, Sugu aliitaka serikali iache kuwahadaa wananchi kwa kutumia nguvu kubwa kuonesha mafanikio ya serikali katika vituo vya runinga wakati wananchi wana hali ngumu ya kimaisha.

“Kama utaangalia mafanikio ya nchi yetu kwenye runinga unaweza kusema tumepiga hatua kubwa katika kilimo, lakini niwaambieni hali ni mbaya kwa wakulima na nilifikiri serikali inaweza kuwa ya kiungwana na kuelezea matatizo halisi yanayowakabili,” alisema Sugu.

Aliongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuelezea mafanikio yasiyokuwepo, na haijulikani fedha zinazotumika kulipia matangazo hayo zinatoka katika mfuko gani.

Sugu alisema hali ilivyo sasa ni wazi CCM wanaomba Mungu 2015 isifike kwa kuwa wanajua mwaka huo ndiyo mwisho wa safari ya muda mrefu waliotumia kuwanyima maendeleo Watanzania

Monday, January 21, 2013

Kigoda urges developing countries to examine environmental standards

Dr Abdallah Kigoda

Developing Countries have been urged to observe deteriorating world environmental standards by minimising the undesired effect resulting from human activities.
The Minister for Industry and Trade, Dr Abdallah Kigoda, made the remarks recently when opening a three-day workshop on Life Cycle Assessment (LCA) and ISO/TC207/Chair Advisory Group (CAG) meeting in Arusha.

A statement issued by Tanzania Bureau of Standard (TBS) quoted Dr Kigoda as saying that for developing countries, environmental standards pose daunting challenges especially when they seek to export products to international markets, adding that the issue of standards comes in as a strong competitive tool.

“Developing countries’ economies are dominated by SMEs which have to grapple with a whole range of rules and regulations for the export market in order to succeed and they have to compete equally with foreign products in which again the issue of standards is vital,” he insisted.

The minister further said the issue of standards, both their formulation and implementation is always important since at the end it touches every single person on earth be it in the developed or developing countries.

He said Tanzania like many other countries in Eastern and Southern Africa is also a member of the World Trade Organization (WTO), which considers international standards as a fair criteria for trade facilitation and for this reason countries should strive to comply with international standards.

For his part TBS acting Director General Leandri Kinabo said a workshop on LCA is a testimony of stakeholders’ commitment and support on the initiative to promote environmental standardisation activities worldwide.

He said the workshop on LCA and the ISO/TC 207 CAG meeting will be a milestone towards sustainable development in the region as well as at the global scale.

LCA is a technique of assessing environmental impacts associated with all the stages of product life, from resource extraction to disposal phase. It is one of the subcommittees under the ISO/TC 207 which deals with environment management matters.

TBS in collaboration with International Organisation for Standardisation through ISO/DEVCO organised the workshop which drew participants from Malawi, Botswana, Burundi, Congo-Brazzaville, Eritrea, Kenya, Lesotho, Mozambique, Namibia, Burundi, Seychelles, Swaziland, Uganda and the host Tanzania.

The CAG meeting which encompasses all leaders of the different subcommittees was established by Technical Committee (TC) 207 of ISO in 1993. It identifies issues, holds preliminary discussions on how to address them, and makes recommendations through the chair of ISO/ TC 207.

The scope of committee is to promote standardisation in the field of environmental management standards and tools in support of sustainable development.

Why our informal sector needs more recognition

The recently published report on Dar es Salaam’s environment, which was initiated by the Environment Division of the Vice President’s office, had more other findings apart from the revelation that the city is seriously polluted. For example what is also unearthed about the informal sector is too important to be taken lightly.

The data in the report show that about 46% of Dar residents are unemployed, while 95% of those working are in the informal sector. A mere 5% of those working are in formal employment.

Given the fact that much is being said about informal employment, most of us today understand what kind of people belong to this category. They include tailors, welders, small traders, food vendors, cobblers, freelance photographers, brick makers, saloon operators and musicians.

The list of informal sector activities which most urban dwellers engage in for the sake of survival is as long as it is interesting.

Informal employment is not just an urban practice. There are all sorts of self employed workers in rural areas, including primary and secondary school leavers who prefer petty trading to farming, and other informal sector undertakings. The rural informal sector seems to grow significantly year after year, as is the case in the urban environment.

What does this kind of scenario imply? To put it simply, all signs indicate that the sector has a unique role to play in the development of underdeveloped countries like ours. Research has established that the contribution of the informal sector to the total national wealth produced and services provided is substantial.

We are told that in Tanzania the sector contributes above 32% to the country’s GDP. The rising youth unemployment is still somehow manageable today, thanks to the informal sector window.

What would be happening in a city like Dar es Salaam or Mwanza today if thousands of youths who are earning a living by offering motorcycle passenger services, running kiosks, selling ‘mitumba’ in open markets etc., were completely idle?

Your guess on the above question is probably as good as mine, but chances are that the rate of urban crime in our midst would have been worse in the absence of the informal sector safety valve.

One would argue that this is another major reason why informal sector activities must be taken seriously, for the good of those who earn an income from it, those who benefit from the services provided, as well as the wider public which enjoy more security as an indirect benefit.

Yet more questions on the informal sector still arise, and beg urgent answers. Is the informal sector really recognised and appreciated? If it is, are adequate efforts being made to improve it in the interest of those engaged in it and society as a whole?

Admittedly, some research on its magnitude and impact to our society has been conducted by several institutions, including the Research on Poverty Alleviation Programme (REPOA), as well as academicians in other local universities. These deserve a pat on the back for taking time to study this vital area involving people determined to employ their energy and determination in order to survive or get out of poverty - if conditions allow.

Recommendations have been given on how to improve the sector but, unfortunately, there are no visible signs to show that it is improving appreciably. Most of those engaged in it are not making much progress and its potential to country’s development is not fully harnessed.

The informal sector continues to experience the same problems they have had for decades. Lack of capital continues to haunt small entrepreneurs, despite the fact that they are not normally asking for a big amount to promote their small businesses. It is due to this poor funding that the International Labour Organization (ILO) consider most informal sector activities as survival one with no future

Some face licensing setbacks when they decide to be more formal in their business approach. Being unnecessarily harassed is part of life for some citizens who depend on informal sector activities for their livelihood. The list is long.

You have those who suggest that may be there is need to have a full ministry to handle and promote the informal sector. Probably they have a point

Ophir Energy agent threatens Zitto Kabwe

Kigoma North Member of Parliament Kabwe Zuberi Zitto has received a demand notice from one Moto Mabanga – commonly known as a fixer -- ordering the legislator to refute allegations he made in Parliament last November.

The demand notice comes about two months since the outspoken MP tabled in Parliament a private motion calling for investigations on some Tanzanians believed to have stashed away billions of shillings abroad -- especially in Switzerland, New Jersey and Cayman Islands as well as Mauritius.

In his private motion, Zitto said he believed some Tanzanians with offshore bank accounts made money from corruption deals and tax evasion.

According to Zitto, the yet unnamed individuals made ill-gotten money through procurement of military hardware, as well as energy and mineral deals.

But Mabanga wasn’t amused when the MP specifically nemed Ophir Energy, an oil exploration firm, as one of the companies that dished out hefty bribes to government officials so that it could be awarded three oil and gas exploration blocks between 2004, 2006 and 2007 -- and that he (Moto Mabanga) was the fixer who facilitated the award of licences for the oil explorations.

In his private motion, Zitto had said that in 2004 an 2005 a prominent South African politician, Tokyo Sexwale, made a business trip to Tanzania bringing with him two friends before he set up a firm known as Ophir Energy Tanzania Limited – which now owns blocks 1, 3 and 4 off the Indian Ocean in the Southern parts of the country.

He further stated that Sexwale was introduced in the country by a Congolese fixer known as Moto Mabanga, but in the demand notice issued to the opposition MP, Mabanga claims that Zitto lied about the man’s nationality.

According to Zitto, in his notice, Mabanga agrees that he indeed facilitated Ophir Energy to get oil exploration licenses in the country but insists that the deals were clean.

Mabanga asserts further that he never bribed any government officials to secure the oil deals in Tanzania.

However, Zitto raises serious doubts, saying, “if indeed he ( Mabanga) did facilitate Ophir Ernegy to strike oil deals in the country why then doen’t he have any shares in any of the oil companies now?”

However, The Guardian on Sunday has not been able see the copy of the demand notice issued to the opposition legislator.

But asked if he would bow down to Mabanga’s demands that he refute the allegations, he brushed it aside and retorted via an email message, “I won’t … this guy’s dealings must be investigated.”

However, Zitto says that the Clerk to the National Assembly had since informed Mabanga’s lawyers about the immunity granted to Tanzanian MPs when discharging their responsilities in the House.

This means that even if Mabanga were to take the matter to court he may hit a snag due to the immunity that Tanzania MPs enjoy.

“What is clear now is that Moto mabanga has confirmed through his demand notice he was a ‘deal sweetner’ for oil blocks in Tanzania. Authorities in Tanzania must investigate the dealings of this person,” Zitto added.

When tabling the private motion last November in Dodoma, Zitto told the House that the Global Financial Integrity (GFI) report of 2008 showed a total of US$8 billion had been stashed in foreign banks abroad between 1970 and 2008.

In June, 2011 the National Bank of Switzeland released details of people holding bank accounts in which it was revealed that Tanzanian individuals stashed away some US $196 million (Sh 314 billion) there.

It was then that the government conduct thorough investigation to establish the identity of Tanzanian personalities holding offshore bank accounts and the amounts preserved.

The government agreed to carry out the assignment and report back to the parliament in April this year.

Moto Mabanga is a well known fixer in Africa who has played many roles in enabling multinational investors to secure ‘smooth’ investments in many countries -- including Tanzania and the Democratic Republic of Congo

Govt given Stiegler`s Gorge power proposal

Implementation of a huge Stiegler’s Gorge Power is becoming a reality after a report and proposal of development of the project being presented to the government at the weekend.

The proposal presented in Dar es Salaam follows a Memorandum of Understanding (MoU) of the long awaited project between the Rufiji Basin Development Authority (RUBADA) and Odebrecht International, a reputable dam construction company in the world six months ago.

“This is a very crucial stage,” the RUBADA Director General, Aloyce Masanja told journalists after receiving the proposal at the event witnessed by top Odebrecht officials, government of Tanzania officials and RUBADA management and members of the Board of Directors.

According to Masanja, the proposal will now give a clear picture on the implementation of the project.

The proposal touches mainly on Power Market Overview, Engineering Studies and Technical Proposal, Preliminary Social-Environmental Evaluation, Key Stakeholders, Stage 1 Risk Analysis and Financial Structure and Proposed Business Plan.

According to Masanja, the project financial requirement is over USD 2 billion, but the figure may vary depending on the technology to be agreed at a later stage.

RUBADA, as a public institution is allowed by law to generate and supply hydroelectric power in the basin and will partner with Odebrecht, a private entity in a form of Public Private Partnership (PPP).

“The project is a multipurpose by nature in the sectors of agriculture, energy, fisheries, flood control and tourism,” he said.

Once completed, the project will have the potential to produce 2100 MW.

The Brazilian company reviewed Feasibility Studies that were earlier done by a Norwegian company, NORCONSULT in 1980 on a similar project but shelved.

The next stage after reviewing the proposal will be designing and doing Environmental Impact Assessment (EIA) while the third stage will be commencement of construction.

For his part, the company’s New Business Director, Fernando Soares said that his company understands the importance of the project, not only for Tanzania but for the whole region.

“We are proud to be part of such important endeavor,” he said.

He said that Odebrecht can provide great value to their clients bringing the necessary engineering, and construction expertise, as well as proven local knowledge and motivation to pursue a well-balanced contractual relationship.

The Chairman of the RUBADA Board of Directors, Prof Raphael Mwalyosi said the Brazilian company has done a great job.

“We are very happy, they have done a great job according to our expectations,” he said.

For his part, the Brazilian Ambassador to Tanzania, Fransisco Luz said that his country is very proud that Tanzania has decided to have a Brazilian experience in the area of dam construction.

It is estimated that the Stiegler’s electricity will be among the least costly in Africa, standing at 4 USD cents per a kilowatt hour, including tax.

“There are more than enough reasons for stakeholders to support this project,” he said.

Odebrecht Company Limited is reputed to be involved in big and successful construction of big hydropower projects in the world. It was involved in construction of the world’s second power project found in Brazil with the capacity to produce 14,000 MW. The whole of the Rufiji Basin has the potential to produce 4,000 MW.

Brazil is said to have transformed her economy for the past 30 years from the low income country to a middle economy today. More than 85 per cent of the country’s power comes from hydro sources.

Its portfolio includes more than 58,500 MW in construction works and services in the power sector.



With more than 65 years of experience, developing projects in 25 countries in 4 continents. Odebrecht which has been working in Africa since 1984 employs more than 20,000 people and has successfully delivered projects in nine countries.

Gesi kuiangusha CCM

• Wabunge wakamia mjadala bungeni

NEEMA ya gesi iliyovumbuliwa Mtwara, na wananchi kutaka ibaki mkoani humo badala ya kuisafirisha kwenda jijini Dar es Salaam, imegeuka laana, na sasa inaweza kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 baada ya wananchi kuanza kupoteza imani nacho, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mikindani, Ali Chinkawene ndio vinara wa kampeni za kupinga gesi hiyo kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, na wamejitokeza hadharani kupinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba wakazi wa Mkoa wa Mtwara hawapaswi kuzuia.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wiki nzima sasa, umebaini kuwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambao wengi ni wafuasi wa CCM, wamepoteza imani na chama hicho.

Baadhi ya wabunge wa mikoa ya Mtwara na Lindi ambao wako jijini Dar es Salaam wakihudhuria vikao vya kamati za Bunge, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kwamba wana-CCM katika mikoa hiyo, wamepoteza imani na chama hicho kutokana na kauli za viongozi wao wanaotumia vitisho kutaka gesi hiyo isafirishwe kwenda Dar es Salaam.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Murji, alisema juzi kuwa msimamo wake wa kupingana na Rais Kikwete uko pale pale na kusisitiza kuwa yuko tayari kutimuliwa ubunge kuliko kuachia mradi huo wa gesi upelekwe Dar es Salaam.

Rais Kikwete katika salamu zake za mwaka mpya wa 2013, alisema Mtwara hawana haki kuzuia gesi hiyo kwani rasilimali inayopatikana popote katika nchi hii ni mali ya taifa, na hutumika kwa manufaa ya taifa na si mali ya watu wa pale ilipogundulika au pale shughuli inapofanyika.

Akionesha dhahiri kupingana na Rais Kikwete, Murji alisema serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara badala ya Dar es Salaam.

Alisema: “Tulipoona hali inakuwa tete, niliitisha kikao cha Kamati ya Siasa kujadili nini msimamo wa chama katika hili. Kamati ya Siasa wakasema hawawezi kukisemea chama kwa sababu chama ni wanachama, hivyo nikaitisha kikao cha Halmashauri Kuu ambapo pia tuliwaalika mabalozi wa mitaa.

“Katika kikao hicho, wajumbe walipinga kwa nguvu zote suala la gesi kupelekwa Dar es Salaam. Wakaniambia niseme msimamo wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale masilahi ya wana-Mtwara yatakapowekwa wazi na serikali na huo ndio msimamo.”

Alisema msimamo huo si wake binafsi, bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho vinavyowakilisha wanachama, na kwamba historia ya mikoa ya kusini jinsi ilivyonyimwa maendeleo, ilitumiwa na wajumbe kujenga hoja hiyo.

“Wakati sisi hatuna umeme, hakuna aliyefikiria kutuunganisha kwenye gridi ya taifa… Barabara ya kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam miaka 51 ya uhuru sasa haijakamilika. Lakini bomba wanataka kujenga kwa miezi 18. Hivi kuna Watanzania muhimu zaidi ya wengine?” alihoji mbunge huyo.

Duru za siasa zilidokeza kuwa, kauli za viongozi hao ndio msimamo wa wana CCM ambao baadhi wameapa kwamba kama serikali haitabadilisha msimamo wake, chama hicho kisahau kushinda uchaguzi wowote katika mikoa hiyo.

Wabunge wengine ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walisema wanasubiri kwa hamu mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mjini Dodoma, kwani wamepanga kuzungumzia msimamo wao kuhusu suala hilo.

“Sisi wengine mtatusikia Dodoma. Tumeamua kutetea maslahi yetu na kizazi chetu kijacho kwani kusini hatukuwa na cha kuwaachia, lakini leo tuna gesi. Haitoki Mtwara,” alisema mbunge huyo.

Wakati wabunge hao wakiweka msimamo huo, jana na juzi, wananchi wa wilaya zote za Mkoa wa Mtwara walifanya maandamano kwa lengo la kuendeleza kilio chao cha kupinga gesi yao kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia suala hilo, Mbunge wa Kigamboni, Dar es Salaam, Faustine Ndungulile, alisema kuwa lilionekana dogo, lakini kadiri muda unavyokwenda, badala ya kuwa kipele linaekelea kuwa jipu na mwisho linaweza kusababisha kansa itakayosambaa mwili mzima.

Alisema: “Nimefuatilia kwa makini kuhusu hoja ya wananchi wa Mtwara, lakini vile vile nimefuatilia kwa makini majibu yanayotolewa na viongozi mbalimbali. Kinachoonekana ni kwamba, viongozi hawajipanga vizuri. Kila mtu anasema lake na kila mtu anafanya lake.

“Kwa mtazamo wangu, katika sakata hili kuna mambo mawili makubwa ya msingi. Mosi, maendeleo duni katika mikoa ya kusini ikiwa ni pamoja na Mtwara. Pili, tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Ndungulile.

Mbunge huyo alishauri elimu itolewe kuwashibisha wananchi wa Mtwara jinsi gani watanufaika kimaendeleo na kwa upande wa ajira kwa vijana.

“Kubeza na kutumia hoja za nguvu havitasaidia, badala yake tunahitaji nguvu za hoja zitakazowaelimisha na kuwashawishi wananchi wa Mtwara katika maeneo yafuatayo:

“Ni vigezo gani vilitumika kufikia uamuzi wa kujenga bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini mtambo wa kuzalisha umeme usijengwe Mtwara na kusambazwa kuja Dar es Salaam? Je, mchanganuo wa gharama ukoje?

“Je, upatikanaji wa gesi hii utakuwa na manufaa gani kwa wananchi wa eneo husika? Je, kutakuwa na viwanda vya kusindika gesi vitakavyojengwa huko Mtwara? Je, mikoa inayozalisha itapata asilimia ya mapato ya gesi inayozalishwa katika eneo hilo?

“Je, ajira ngapi zitakazozalishwa na sekta hii, na asilimia ngapi ya ajira zitakuwa kwa ajili ya wakazi wa eneo hili?”

Mbunge huyo alisema suala hili linapaswa kushughulikiwa mapema na kwa haraka wakati likiwa bado ni kipele kwani likishakuwa jipu au kansa, gharama za kulishughulikia zitakuwa kubwa.

Alisema wananchi kuhoji si dhambi wala uhaini kwani uelewa wao umekua na wanahitaji kushirikishwa na kupewa majibu ya kina

Sunday, January 20, 2013

Wildlife authority to be set up in Nov this year.

The Ministry of Natural Resources and Tourism has reaffirmed government commitments towards establishing a state owned wildlife authority later this year.

Deputy Minister Lazaro Nyalandu disclosed the government plan over the weekend, noting that the authority will come into operation in November.

The minister said upon its establishment, the authority will compliment anti-poaching efforts in the country.

Last year the government acknowledged in the House that it was putting final touches on plans to set up the authority, including earmarking its responsibilities.

He said that a task-force on the establishment of the authority had visited the Tanzania National Parks Authority (TANAPA) and Ngorongoro Conservation Authority (NCA) to learn how they operate.

According to Nyalandu, the task-force was able to review operational structures of the two authorities which would enable it to advise on how the new authority should be set up and operate. Responsibilities and structure of the authority would be ready by September, this year.

He said drafting of a bill on establishment of the authority started in October and was completed by December last year.

He explained further that section 8 of the Wildlife Conservation Act of 2009 gives power to the Minister of Natural Resources and Tourism to establish the wildlife authority.

The envisaged law and eventually the establishment of the authority are expected to increase revenues from forests, national parks and game reserves countrywide

Mtwara to receive 0.3 percent of gas revenues

Gas reserves in the country are already causing domestic upheaval even before actual extraction as residents of Mtwara raise concern that they were being ignored in the development project in favour of Dar es Salaam where the Mtwara extracted gas is to be piped to.

However, addressing journalists yesterday in Arusha, the deputy minister for Energy and Minerals George Simbachawene said: “I don’t see the reason as why people are opposing the project despite the myriads of benefit the country is expected to get…”

The minister added that upon its completion, Mtwara will receive 0.3 percent of the total income that will be collected from the project.

“This is a huge amount of money and there are lots of investors who are waiting for the completion of the project to set up new industries that will employ many of the Mtwara residents…” he affirmed, giving the gas processing plant, cement and fertilizers factories as some of the plants to be built in the region.

According to the minister, the government has all financial resources needed for the project which is to be completed within eight months and a contractor for the project is already on the working site.

“We are interested to see this project start and be completed as soon as possible…” he asserted and asked Tanzanians to be patient.

He described the protest against the project as a politically motivated venture, without any national development agenda, only seeking to cause destruction.

Recently people from Mtwara staged a demonstration against the government’s plan to pump the natural gas to Dar es Salaam.

The protest themed: ‘Natural gas comes before political affiliations’ was organised by eight opposition political parties. Their sympathisers called for the industrial investment to be made in Mtwara and not in Dar es Salaam.

The minister explained that once piped to Dar es Salaam, the natural gas will serve the nation as a whole in a host of development projects including, domestic use as well as to power various production plants and is expected to reduce the cost incurred in importing fuel.

“With these unprecedented climatic changes, natural gas is the most economical and viable way to go…” the minister said noting that upon completion of the project, the country will enjoy about 2,780 megawatts which will have a positive impact on growth.

“It is time we Tanzanians put aside our political differences and built our nation…” the Minister asserted

Mwakyembe to ease Tunduma truck flow.

From right: Trade and Industry minister Dr Abdallah Kigoda, Transport minister Dr Harrison Mwakyembe and Finance Minister Dr William Mgimwa with their host, Tanzania Truck Owners Association Chairman Seif Ali Seif, head to conference room at Ubungo Plaza in Dar es Salaam at the weekend where Dr Mwakyembe was chief guest to the TATOA annual general meeting. (Photo: Khalfan Said)

Transport Minister Dr Harrison Mwakyembe has assured members of the Tanzania Truck Owners Association (TATOA) that he will take action against the slow pace of truck movement at Tunduma border post.

He was responding to remarks made by TATOA chairman, Seif Ali Seif at the annual general meeting of the association held over the weekend in Dar es Salaam.

The TATOA chairman said, truck movement remained one of the major hurdles in the transport sector, saying: “Initially Tunduma border post was designed to serve approximately 40 to 50 trucks per day at that time, but currently more than 400 to 500 trucks are crossing that point daily,” noted Seif.

He further said trucks bound for Zambia and DRC spent more than six days to cross the border due to the heavy traffic and documentation procedures adding that, the infrastructure at Tunduma border post is outdated and overwhelmed by the influx of trucks.

Minister Mwakyembe, who was the chief guest said: “I have received your critical concern on truck dwell time at the border post. I promise that I will make a close follow up in collaboration with other parties to make sure this hitch is sorted out.”

On August 29, last year during the meeting between the minister for Trade and Industries, Dr Abdallah Kigoda and TATOA executive committee, the association proposed opening ten gates at Tunduma border point instead of the current single gate. “Among the 10 gates, we propose that two be for passengers, three for dangerous goods such as petroleum products which by their nature are not allowed to stay for long hours and the remaining five gates for containerized cargo,” TATOA told Dr Kigoda.

Meanwhile, Dr Mwakyembe has praised TATOA for being one of the leading players in the country’s economic development, noting that last year, a total of 40 million tons of cargo were transported, three million being transit cargo to or from the neighboring countries.

“Statistics show that there has been an increase of 400 percent of cargo transported to the neighboring countries from 2006 up to 2012. This achievement is the outcome of the good leadership of TATOA and they deserve member’s recognition and on behalf of the government I would like to congratulate you for your commendable leadership,” applaud Mwakyembe.

Dr Mwakyembe also had promised to take into consideration the stalemate request from TATOA, asking the government to hand over the Kihonda Driving Institute in Morogoro to be run by TATOA. “I have received by two hands your request to run Kihonda driving institute, I personally believe that, it is important to have competent drivers who have attended proper driving training, I will sit with your chairman to see what we can do and also to meet with the concern minister,” he said.

The minister for Industries and Trade Dr Abdallah Kigoda concurred with TATOA that the challenges facing the transport sector need an urgent intervention. “Surely these weighbridges and roadblocks are among the Non Tariff Barriers (NTBs). They should be reduced to increase efficiency and save time in transportation of goods,” he said

Dr Kigoda also advised TATOA to come up with cost-effective analysis if they want their proposal on the abolition of bothersome levies such as city service levy. “We need a win-win situation without harming any side. The government needs tax and you need profit,” he stressed.

For his part, the minister for Finance, Dr William Mgimwa praised TATOA, for their commendable role in the country’s economy. “Statistics show that, transport sector plays a pivotal role in providing employment for our people, as well as being a large contributor in taxes, ” he said.

According to Dr Mgimwa, the transport sector is very important in implementation of the economic development of the country and the government recognised the role of TATOA in this fact.

Meanwhile, TATOA general meeting has elected eight new members to serve as the executive committee,

According to TATOA’s constitution, the executive members have also re-elected the former chairman, Seif Ali Seif to the post, and Angelina Ngalula as the vice chairperson.

Other executive members include Zacharia Hans Pope, Elias Lukumay, Omar Kiponza, Alkarim Dawood, Alistair James and Ally Azim Dewji.

Major land dispute brewing in Kibaha

Kibaha District is headed for a major land dispute after the sticks used as beacons to identify plots at Disunyala area in Kibaha District, Coast Region, were eaten up by ants.

More than 150 plots surveyed at the area five kilometres off Dar es Salaam-Morogoro Road near Mlandizi, will need fresh demarcation to avoid conflicts that might arise between the new owners over borders.

“It’s like is walking over unmarked graves,” said Mohammed Musa, one of the people who went over the weekend to be shown his family’s plot.

This reporter visited the site where he witnessed the small sticks meant to be the beacons that identify the surveyed plots, some of which have been eaten by ants, while others have apparently been removed by unknown people.

Only one beacon Number ZFA 429 was seen in place in the area, leaving many of the people who went to see their allocated plots fearing that some dishonest developers might take advantage of the situation to create their own demarcations.

This could result into conflicts, as land issues become more sensitive, they pointed out.

A land officer in-charge of the Disunyala plots allocation, Lenard Mhongole acknowledged the poor demarcation of the plots in the area, attributing it to people who might have uprooted the wooden beacons for domestic use and most probably the charcoal makers.

He said because the area was yet to be developed, some of the vandals might have seized the opportunity, especially since the area was un-occupied.

Owners of the more than 150 plots were allocated their plots after paying all dues to the Kibaha District land office.

The Kibaha District Executive Director, Tatu Selemani told this paper over the telephone that the work of demarcating the plots was carried out by a Dar es Salaam-based firm called Ardhi Plan and that she thought all was going well at the site.

“What we know up to this moment is that all is well because we have not received any complaint from the firm we assigned the work,” she said while asking this reporter to contact the firm.

When contacted, one of the firm’s officials who gave one name of Liombo said he was not in a position to respond to this reporter’s questions over the phone.

A motor cyclist famous for sending potential developers to the Disunyala site from Mlandizi, Rashid Abdul, told this reporter that many of the people he had taken to the plots came back frustrated.

“Some of them even think they have been conned, after they were not shown their plots because the beacons had been up-rooted,” he told this reporter.

The problem started brewing last week when officials of the Land Division in the district opted to keep mum over persistent requests by owners seeking to be allocated their plots after paying millions of shillings for them.

Potential developers paid between 2m/- to 6m/- for the plots since October last year, but the allocation started only last week.

The Acting District Land, Natural Resources and Environment Officer, Frank Mwalembe summoned at the DED’s office admitted that there were some hitches on the whole issue of allocation of the plots, but said the issue would be solved cordially “very soon.”

A 600 square-metre plot in Disunyala costs a sum total of 3m/-, of which 1,667,012/- is deposited into one David Robert Makange’s account number 01523158487000, leading many payers to ask why a private person was being paid when Kibaha district officials were issuing the title deeds.

It was later revealed that Makange was the former owner of the area which was being demarcated into plots and that the Kibaha District was only facilitating the exercise, of course with levy remitted by the owner of the area.

Out of the 3m/- paid, 979,039/- is paid into Ardhi Plan account number 0150029829003 at the CRDB Bank. There was also an outcry on the hiring of a private surveyor while there were experts in the ministry of Lands to do the job.

Another 300,000/- was to be paid into the Kibaha District Council Account No. 2121200191 – NMB account called ‘ Own Source Collection Account’ and 49,950/- to be paid into CRDB account number 2121200195 named ‘ Miscellaneous Deposit’.

A notice signed by one H.K. Kidimani on behalf of the Kibaha District Council asked people wanting the plots to hand over the various bank paying slips to the Lands office for it to process the title deeds

CAG ataka ofisi yake iwe huru

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amependekeza kuwa ofisi yake iwe taasisi ya kujitegemea ili iwe huru kufanya kazi bila kuingiliwa na idara nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kutoa maoni ya ofisi yake katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema watumishi wa idara hiyo wanapendekeza ofisi yake iwe taasisi inayojitegemea.

Utouh, alisema kuwa idara hiyo inafaa kuwa kama ilivyoundwa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) au Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuweza kufanya kazi zao kwa uhuru huku wakiweza kuajiri.

Akitolea mfano, CAG alisema wakati mwingine huitaji kuajiri, lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa kuwa kuna taratibu zinazowahitaji kuandika barua kwanza serikalini.

Aidha, mwasisi wa kupigania uhuru nchini aliyewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini, George Kahama, naye alitoa maoni katika ofisi za tume hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kile alichokieleza.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alipoulizwa juu ya maoni yaliyowasilishwa na Kahama aligoma kuzungumza

Saturday, January 19, 2013

Msigwa aifyatua Ikulu

• Aituhumu kuwapa vyeo majangili

BAADHI ya maofisa wa taasisi nyeti za serikali ikiwemo Ikulu, wametuhumiwa kula njama kuwaficha watu waliotuhumiwa kuhusika na vitendo vya ujangili na wengine kuwapandisha vyeo vikiwemo vya ubalozi.

Tuhuma hizo zimetolewa jana na Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, alipozungumza na waandishi wa habari na kueleza kusudio lake la kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuunda tume ya kuchunguza sakata zima la tuhuma za ujangili.

Hata hivyo, mbunge huyo hakuweza kutaja majina ya maofisa wanaotuhumiwa, lakini akafafanua kuwa alipokuwa katika kamati ndogo ya kufuatilia utoroshwaji wa twiga, kuna majina ya watu yalitajwa kwa ajili ya kuchunguzwa na ikibidi wachukuliwe hatua, lakini kilichofanyika ni wahusika kupewa vyeo vya utumishi, ukiwemo ubalozi.

Msigwa alisema tayari Januari 8 mwaka huu katibu wa Bunge amemtaka awasilishe maelezo ya hoja yake kwa Spika kufuatia barua aliyoandika Desemba mwaka jana juu ya dhamira ya kuwasilisha hoja binafsi.

“Nitaomba iundwe kamati teule ya Bunge kufuatilia huu ujangili unaoendelea nchini, kwani tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa robo ya pembe na meno ya faru na ndovu duniani zinatoka Tanzania.

“Idadi ya tembo wanaouawa ni wastani wa 67 kwa siku, na hali hiyo ni hatari kwa rasilimali asili za taifa na pia inahatarisha maliasili na urithi wa nchi,” alisema.

Alisema mtandao wa ujangili nchini ni mkubwa kuliko inavyofikiriwa, na kwamba hata wanaojitoa mhanga kushughulikia hali hiyo maisha yao yanakuwa hatarini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alipoulizwa juu ya tuhuma hizo, alikana kuhusika kwa Ikulu, lakini akadai kuwa mtandao wa biashara hiyo ni mkubwa, na kwamba mazingira yaliyopo yanatia shaka kuwa baadhi ya viongozi wanahusika.

“Haiwezekani kontena linapitishwa bandarini Dar es Salaam bila mtu yeyote kujua nini kimebebwa, halafu ufike Indonesia au China ndipo pembe hizo na meno yakamatwe, kuna kuzembea hapo na rushwa ndani yake,” alisema.

Alikiri kudokezwa na Mchungaji Msigwa kuhusu kusudio la kupeleka hoja binafsi na kudai kuwa ni hatua nzuri inayotokana na ukereketwa na uzalendo alionao kwenye rasilimali za taifa.

Hata hivyo, Kagasheki alisema idadi ya tembo inayotajwa kuuawa nchini si ya kweli kwa kuwa juhudi za udhibiti zinazofanywa na wizara yake zimepunguza kasi hiyo hadi kusifiwa na Jumuiya ya Ulaya.

“Hizi pembe za ndovu zinazokamatwa si kwamba tembo wote wameuawa wakati huu, haya ni makusanyo ya muda mrefu huko nyuma. Lakini vile vile watu wanapaswa kuelewa kuwa tembo wengi si kweli kuwa wanauawa Tanzania,” alisema.

Kagasheki alisema kuwa pembe hizo na meno ya tembo yanatoka kwa wingi katika nchi za Malawi na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako wanyama hao wanauawa zaidi, lakini usafirishaji wake unapitia katika bandari ya Tanzania.

Alisema nchi hizo hazina bandari na hivyo hutumia Tanzania hali inayofanya nyara hizo zinapokamatwa nje ya nchi kuonekana kuwa zimetoka hapa, hivyo kuonekana kama kitovu cha biashara hiyo.

Lembeli apigilia msumari

Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imepigilia msumari kwa kuanika namna hoteli za kitalii zilivyoongoza kwa hujuma.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam jana, alisema wamiliki wa hoteli hizo wamekuwa wakiilipa serikali dola 4 tu, kwa kila mgeni wanayempokea, wakati wao wamekuwa wakitoza dola 350.

Lembeli alisema hujuma hiyo, imetokana na mikataba ya ovyo iliyopo, na hivyo akaagiza serikali kuwasilisha mikataba yote ya hoteli zilizoko ndani ya hifadhi, kuchunguza kwanini zinalipa kiasi kidogo cha fedha ilhali wanakusanya zaidi.

Lembeli alisema kumekuwepo na mzozo na malumbano katika hoteli za Ngorongoro, Seronera na Noro, ambazo kwa mujibu wa mikataba iliyopo pesa inayolipwa dola 4 ya kila mgeni kwa siku ni ndogo.

“Tulipowahoji walisema kuwa mikataba inawafunga. Je, ni kwanini watu hawa wanatengeneza pesa ndani ya hifadhi, lakini hawachangii kile wanachokipata?” alihoji Lembeli.

Alisema kuna mchezo mchafu unafanywa ndiyo maana zilitolewa kwa bei ya kutupwa, kiasi kwamba kama Mwalimu Julius Nyerere angefufuka leo na kushuhudia ufisadi huo angetoa machozi.

Alishangaa kuona kuwa, mtu anayeweka ‘tenti’ ndani ya hifadhi analipa dola 60 kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa) iweje hoteli hizo kubwa zilipe dola nne mpaka sita?

Katika hatua nyingine, Lembeli amemshukia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira kwamba ndiye tatizo kubwa la wananchi kuishi katika maeneo ya malisho ya wanyama.

Lembeli aliyasema hayo jana mbele ya Waziri Kagasheki na Naibu wake Lazaro Nyalandu wakati wa kujadili ripoti ya wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.

Alisema Wassira ni tatizo na amemtaka kukaa naye ili wananchi katika jimbo lake waache kuingia katika maeneo ya Ushoroba ambayo ni sehemu sahihi ya malisho ya wanyama katika hifadhi hizo

Sunday, January 13, 2013

Bagamoyo gets USD50,000 to boost ecological tourism

The Environmental Development Fund has granted USD 50,000 to Bagamoyo Town Municipal for the implementation of its strategy to improve tourism in nine countries in Africa.

Speaking during the launching of the Ecological tourism project, Bagamoyo District Commissioner Ahmed Kipozi said Bagamoyo residents should feel proud of the project as it is an opportunity for employment, but also could represent the country in international arena especially in tourism.

He called on the relevant authorities to put the fund to the use intended by the donors in order to preserve the good image of the country and also embrace the employment opportunities hence contributing to the development of the country at large.

Kipozi called for transparency and involvement of the people and tourism specialists at all stages of the implementation of the project’s goals.

For his part, Bagamoyo Municipality planning Officer Clemence Mkusa said that strategies of the implementation of the project shall build capacity among the people in improving the current environment in the municipality.

Apart from building capacity, he said that it could bring new skills to various groups dealing with tourism activities, tour guides and fishermen along the Indian Ocean thus helping to the preservation of the natural resources around the Ocean.

Bandits terrorise Dar`s Kigamboni hostel zone

















A sizeable number of students from various universities, colleges and schools putting up at private hostels at Kigamboni in Dar es Salaam are living in deep and pervasive fear for their lives and the safety of their property.

This follows a wave of raids at the hostels, most often at night, believed to involve criminal elements from neighbouring areas hunting for laptops, mobile phones, money and various other valuables.

Sources say two of the raids have left at least two male students seriously injured, one nursing machete wounds and admitted to the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI). One of the students hurt is said to be from the main (Dar es Salaam) campus of the Institute of Finance Management (IFM).

This paper has it on good authority that representatives of the IFM administration have on several occasions toured parts of the Kigamboni suburb commonly raided by the bandits and held talks with local residents, but this does not appear to have helped.

The exact number of hostels raided and students accommodated there has yet to be established, but Dar es Salaam Special Zone Police Commander Suleiman Kova is said to have visited the terrorised areas earlier this week to assess the situation on the ground.

Impeccable sources told this paper that armed police officers have since that visit been deployed to the hostel sites to ensure law and order and thus reassure panic-stricken residents about that the situation was under control and there was no cause for alarm.

“Commander Kova toured the area some three or four days ago for a first-hand account of the situation after he had learnt of what was going. Soon after, we discovered that there was an especially heavy presence of regular and other police personnel on day and night patrol,” said a Mwalimu Nyerere Memorial Academy student accommodated at one of the half-dozen or so hostels in the area.

“But this has not stopped students from taking away their laptops, mobile phones and other valuable items for safe custody at their respective homes and other places of their choice,” she added.

The student, who sought strict anonymity “for fear of my safety”, said her hostel is one of four or five along what is popularly known as Serengeti Street, “which has been targeted by the bandits on three occasions recently and where we are all scared of moving around except when we are in groups”.

“It is very awkward for a university or college student to be forced into moving without a laptop or a mobile phone, as these gadgets play a decisive role in academic life. We hope the police patrols will remain in force for a long enough time for lasting peace to prevail,” she added.

Another student, who said his hostel was raided once last month, expressed fear that things could worsen unless security is intensified through sustainable intervention by law-enforcement agents and through community policing.

“We are fortunate that, until now, the gangsters have only targeted money and technological gadgets. But one day they may choose to inflict even more harm, including resorting to rapes and killings,” he added, calling for immediate consultations between government and university authorities on ways to solve the problem once and for all.

The student noted that one of the parts of Kigamboni especially notorious for the raids is Tungi, “an area where soldiers could be easily deployed to complement police efforts to restore peace and harmony”.

Contacted, Commander Kova refuted to have visited the hostels saying that it was not his work adding that he has his commanders who could do the work.

The Temeke RPC Englebert Kiondo when contacted said he planned to pay an abrupt visit to the area so that he could get sufficient information on how to deal with the criminals.

"I received a phone call yesterday from a person identified as one of the students living in one of the hostels at Kigamboni informing me about the crime…I am planning to visit the area,” he said.

He said he would seek more information from the Officer Commanding District before visiting the hostels which have been affected by the crime.

Such raids have also been reported in other private hostels around the city, which boasts the highest number of higher institutions of learning, but limited on-campus accommodation facilities.

Over 13,000 pupils shun ward secondary schools, says report

Over 13,000 pupils in Kinondoni District who were selected to join ward secondary schools in the past three years opted for private ones because parents and guardians have no confidence in the quality of education offered at the schools, a report has said.

A report issued over the weekend by Kinondoni District Education Officer (Secondary Education), Omath Sanga and submitted to the District Executive Director (DED), copy of which was availed to The Guardian shows that a total of 13,275 pupils did not report to the schools they were selected to join in the past three years.

Sanga said that in 2010 the number of pupils who did not report to the schools was 5,112 out of 15,700 who were selected.

In 2011 of the selected 14, 823 only 10,128 students joined ward schools while the remaining 3,695 opted for private schools.

Last year of the 13,955 chosen to join the secondary schools, only 9,487 reported, while 4,468 failed to do so.

Meanwhile education stakeholders have blamed the government for the poor performance of Form Two students saying that it was due to standardisation of the pass marks.

The stakeholders’ reactions come a few days after the Ministry of Education and Vocational Training released results indicating over 130,000 students are required to redo the examinations.

Speaking in separate interviews they said that standardization of pass marks has allowed pupils with low performance to join secondary schools.

Juma Mabuba a teacher at Bundikani Secondary School in Coast Region said students selected to join secondary education are of low academic capacity, but that the government is pushing them to fill the gaps in secondary schools.

He said almost 80 percent of students joining secondary schools don’t know how to read and write, creating a burden for teachers who have to start teaching them how to read and write instead of proceeding with the syllabus.

Mabuba however called on the government to raise the pass mark from 75 to 150 out of 400, so as to get better and qualified students to join the secondary schools.

He challenged district education officers’ programme of forcing teachers to run separate classes for better students and poorly performing ones as worsening the situation, since the poor performers lack support from the better pupils.

However, Annestazia Athuman a Form Two student at Mwanalugali secondary school blamed teachers and the government for the recurrence of teachers’strikes which affected their performance.

Athuman said the strikes affected them because teachers were not committed to teach since their demands have not been met.

“After the government forced teachers to teach while it has not resolved their grievances, they opted for go-slow she said.

For his part, President of the Tanzania Teachers Union (TTU), Gratian Mukoba said Dar es Salaam region deserves to lead in poor performance in the recent Form Two results because students are over-crowded, with almost 2000 per class, making it very difficult for a teacher to manage the burden.

He said the government should take note of the students claims that the teachers’ strike has contributed to the poor performance, and find a solution.

On Friday last week, the Deputy Minister for Education and Vocational Training, Philipo Mulugo said over 136,000 Form II students have failed the national examinations and are required to redo the exam in 2013 academic year.

The government reinstated the examinations were last year as one of the measures to contain cases of massive failures of students in the Form IV national examination

Pinda: Uchumi wa Tanzania utakua maradufu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema uchumi wa Tanzania utaendelea kukua maradufu kutokana na mifumo bora ya uwekezaji iliyopo, hali itakayosaidia pia kushindana katika soko la Afrika Mashariki.

Pinda alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa duka la kusambaza bidhaa za Beko kutoka Uturuki, zikiwemo televisheni, friji na majiko ya umeme.

Alisema fursa muhimu ndizo zinazovutia wawekezaji kuja nchini na pato la nchi kuendelea kukua maradufu.

Alisema mara zote Tanzania imekuwa katika kutafuta masoko na wawekezaji, hivyo kuzinduliwa kwa duka hilo ni ishara kuwa nchi imepiga hatua kwenye maendeleo.

“Uwepo wa Beko ni matunda bora ya serikali yetu… rais wetu alitembelea Uturuki na alikutana na rais wao huko na kuhimiza wawekezaji kuja nchini. Hii ni moja ya matunda ya ushirikiano katika kukuza uchumi,” alisema Pinda.

Aidha, Pinda aliishauri Kampuni ya Modern Holdings (EA) Limited, inayosimamia bidhaa za Beko nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufungua maduka mengi zaidi nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Anselm Minja, alisema bidhaa za Beko zitapatikana nchini kote kwa kufungua maduka sehemu mbalimbali kama walivyoombwa na Pinda.

Mbunge, Magufuli wampinga Mwakyembe

MBUNGE wa Ilemela mkoani Mwanza, Highness Kiwia (CHADEMA), ameungana na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kupinga agizo la Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuhusu kufungwa barabara kuu ya Igombe-Kayenze iendayo katikati ya Jiji la Mwanza.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Kiwia alisema kauli ya Waziri Mwakyembe kutaka barabara hiyo ifungwe ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa jijini hapa, haina tija kwa wananchi kwani hadi sasa hakuna maandalizi yoyote ya upanuzi yanayoendelea.

Alisema kuwa ili barabara hiyo ifungwe, ni lazima serikali ijenge njia nyingine mbadala kwa ajili ya wananchi, na kwamba ni vema wizara hizo mbili za Uchukuzi na Ujenzi zikalipatia ufumbuzi wa haraka sana suala hilo.

Kauli ya Kiwia imekuja siku mbili baada ya Waziri Magufuli aliyefanya ziara ya siku moja jijini hapa, kupinga agizo la Waziri Mwakyembe ambaye hivi karibuni naye alifanya ziara kukagua mradi huo kisha kuagiza barabara hiyo ifungwe mara moja ili kupisha upanuzi huo unaotarajiwa kuchukua muda wa miezi 24.

"Mimi kama mbunge wa Ilemela, naungana na Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli kupinga agizo la Waziri wa Uchukuzi, Dk. Mwakyembe kuhusu kufungwa kwa barabara ya Igombe-Kayenze ili kupisha upanuzi wa uwanja, lakini pia nashangaa mawaziri hawa wanakuja bila kunishirikisha mbunge wa eneo husika,” alisema.

Alisema anamwomba Waziri Mwakyembe asimuelewe vibaya kwa kuwa hapingi kauli yake kwa nia mbaya, bali anakataa barabara kufungwa bila kujengwa njia mbadala ya kuwawezesha wananchi kupita.

Kiwia pia alieleza kushangazwa na mgongano huo wa wizara mbili kuhusu barabara hiyo, akisema inawezekana serikali imetenga fedha za upanuzi wa uwanja huo kisha kusahau kutenga bajeti ya ujenzi wa barabara mbadala wakati wa upanuzi.

Kuhusu mkandarasi wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) aliyepewa kazi ya upanuzi wa mradi huo kuchelewa kuanza kazi kwa mujibu wa mkataba, Kiwia aliitaka Bodi ya Makandarasi nchini (TRB) kwa kushirikiana na serikali kumchukulia hatua za kisheria.

Akiwa jijini Mwanza juzi, Waziri Magufuli alisema licha ya serikali kumlipa mkandarasi huyo zaidi ya sh bilioni 8 kwa ajili ya kazi hiyo, lakini hadi sasa maandalizi yake ni asilimia 30 tu

Dk. Slaa afunguka

• Afafanua chimbuko la mkataba kati ya makanisa, serikali

KWA mara ya kwanza, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameweka bayana chimbuko la mkataba wa makubaliano kati ya serikali na makanisa, huku akiwasihi Watanzania kujiepusha na malumbano yenye hisia za udini.

Dk. Slaa alitoa tahadhari hiyo jana katika ufafanuzi wake aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forum, kuhusu mkataba huo (Memorandum of Understanding - MOU) kati ya Baraza la Kikristo Tanzania, Baraza la Maaskofu Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kuwa amelazima kutoa ufafanuzi baada ya kuona mkataba huo umewekwa kwenye mtandao wa kijamii, huku watu wengi wakiwa wanauzungumzia kwa kupotosha ukweli wa jambo hilo, na kulihusisha na masuala ya udini.

“Kama mnavyoona, mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu, na au kuwa na kila kitu, ‘we need to complement each other’.

“Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila, wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza taifa letu litakuwa hatarini,” alisema.

Alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa, kubomoa ni kazi nyepesi, lakini kujenga tena inachukua muda mrefu, na ni kazi ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa.

Akifafanua historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa, Dk. Slaa alisema kuwa huko nyuma serikali ilitaifisha shule nyingi za madhehebu ya dini.

Kwamba utaifishaji huo uliendana pia na ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati huo shule zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na vitu vingine.

Alisema kuwa kwenye miaka ya 1980, madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo.

Dk. Slaa alifafanua kuwa, mchakato wa mjadala ulishika kasi mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), lilipopitisha azimio rasmi na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na serikali kuanzisha mchakato wa kufanya upembuzi na kutenga ardhi ya shule rasmi, kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini.

“Wakati huo mimi (Dk. Slaa), ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo Desemba1985. Wakati huo madhehebu yaliishakudai yarudishiwe shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana,” alisema.

Aliongeza kuwa serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa, shule hizo zinawahudumia Watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

Dk. Slaa aliongeza kuwa, mawasiliano yalipoanza na serikali, wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, serikali iliomba TEC na madhehebu ya dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri.

“Wakati mchakato huo kwa upande wa elimu umeanza, kulikuwa pia na mgogoro kati ya serikali na TEC baada ya serikali kuichukua Hospitali ya Bugando kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha,” alibainisha.

Kwamba hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani (Misereor).

Alisema kuwa Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na wahisani, walikataa katakata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa shule au hospitali, vituo vya afya na zahanati, kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yoyote.

Wahisani hao walisema hawawezi kuwekeza fedha za walipakodi wao (Ujerumani), lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia dawa na elimu kwa shule ambazo bado ziko chini ya madhehebu ya dini kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama, na kulikuwa na mgomo kila siku kwa madaktari, manesi na watumishi, serikali ikaomba wajadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili.

Mambo hayo ni utoaji huduma katika sekta za huduma za jamii, na kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini.

Lakini kwa kuwa madhehebu ni mengi, wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa sheria.

Hivyo, Waislamu wakawakilishwa na Bakwata, TEC na CCT (kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania), na baada ya mashauriano waliunda chombo hicho.

Alifafanua kuwa kutokana na hali mbaya ya shule, serikali iliomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati kwa zile zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya.

“Nasi kwa upande wetu, kwa nia njema ya kuisaidia serikali, lakini pia kuwahudumia Watanzania, tuliwasiliana na wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo,” alisema.

Katibu huyo aliongeza kuwa, serikali ilipojulishwa ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Anne Makinda, wakati huo akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Hatimaye, serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana mkataba na madhehebu ya dini. Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani, tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduma za jamii,” alisema.

Hatimaye, makubaliano yalifikiwa na ndipo kikazaliwa chombo kipya, Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), chenye sekretarieti yake, hivyo huduma ya Christian Medical Board ya TEC na CCT, ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC.

Dk. Slaa aliongeza kuwa, kwa upande wa serikali aliweka saini Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu wakati huo. Kwamba TEC na CCT nazo zikawekeana na wahisani mikataba yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii

Wednesday, January 9, 2013

Magufuli amsimamisha kazi mkandarasi Tabora

WAZIRI wa ujenzi, John Magufuli ametangaza kumsimamisha kazi mkandarasi wa kampuni ya Progressive Constructions Ltd - Higleig Joint Venture anayejenga barabara ya Songea – Namtumbo – Kilimansera hadi Matemanga.

Magufuli alifikia uamuzi huo jana wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa miradi minne mikubwa iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami mkoani Tabora.

Magufuli alisema kuwa Mkandarasi Progrissive ameshindwa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mkataba, hivyo amesimamishwa huku vifaa vyake vikizuiliwa.

Aidha Rais Kikwete alizindua ujenzi wa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na barabara ya Nzega – Puge – Tabora yenye urefu wa kilometa 114.9 inayounganisha mji wa Nzega na makao makuu ya mkoa huo ambao unaunganisha Tanzania na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi Rais Kikwete alisema kuwa Serikali katika mkoa huo inatekeleza jumla ya miradi mikubwa ya barabara minne yenye urefu wa kilometa 293.9 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la Mbutu.

Naye Mtendaji Mkuu wa Tanroads Injinia Patrick Mfugale, alisema mradi huo unagharimu kiasi cha sh. bilioni 135 na unajengwa na Kampuni za ‘China Communications Construction Company Ltd (CCCC) kwa sehemu ya Nzega-Puge yenye urefu wa km 58.8.

“Huku kampuni ya ‘Sinohydro Corporation Ltd’ inajenga sehemu ya Puge – Tabora yenye urefu wa km 56.10 zote za kutoka nchini China zinazosimamiwa na Kampuni ya ‘SMEC International (PTY) Ltd’ ya Australia,” alisema.

Alisema mradi mwingine uliozinduliwa ni ujenzi wa sehemu ya barabara inayotokea Itigi mkoani Singida kupitia Tabora hadi Urambo ambayo inaenda hadi Kigoma.

“Pia barabara nyingine iliyozinduliwa ni kuanzia Nyahua kupitia Tabora hadi Ndono yenye urefu wa kilometa 127 ambayo inajengwa na makandarasi wawili kwa gharama ya Sh. bilioni 151,” alisema.

Alisema kuwa barabara hizo zitaondoa kilio cha wakazi wa eneo hilo cha kukosa mawasiliano yenye uhakika kwa njia ya barabara za kuwaunganisha na mikoa mingine jirani.

CHADEMA si kuvaa ‘kombati’

NIMEGUSWA sana na mfululizo wa makala za Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto, zinazoendelea kutolewa katika gazeti hili.

Katika mfululizo huo, Jumalipili iliyopita aligusia misingi ya chama hicho akisema ‘fuata misingi; Ujenzi wa CHADEMA imara. Humo alijaribu kugusia ni wapi chama hicho kimetoka kiasia hadi kufikia hatua hii ya kuvuma kila kona ya nchi.

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, anajaribu kueleza jinsi chama hicho kilipigana na kushiriki chaguzi zote tangu mwaka 1995, lakini kikishirikiana na vyama vingine kwenye nafasi ya urais hadi mwaka 2005 ambapo, Freeman Mbowe, aligombea kiti hicho.

Alisema mazingira hayo ya chama cha tano kwa wingi wa kura katika vyama vyote vya siasa nchini ndiyo mazingira iliyoingia nayo CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2005.

“Mazingira ya kukatisha tamaa, kwani ujanja mjini haukuwa kwa CHADEMA; bali CUF au TLP na zaidi CCM. Mazingira ya kijana ukisema upo CHADEMA vijana wenzako wanakuangalia jicho la mshangao na hata kuchekwa,” anasema Zitto.

Kwamba hayo ndiyo mazingira ambayo alirithi Freeman Mbowe, kama mwenyekiti wa CHADEMA.

Alianza harakati zake za kuimarisha CHADEMA kwa kukusanya vijana mbalimbali, wanachama na wasio wanachama.

Vijana hao walitoka makundi mbalimbali ya jamii kama wanafunzi wa vyuo vikuu, waandishi wa habari, wanasiasa kutoka vyama vingine na hata vijana wanaharakati katika NGOs na kwingine.

Zitto anasema mwaka 2004 mwezi Machi, Mbowe akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa tatu wa CHADEMA, hivyo kuwa na mamlaka zaidi ya kuleta mabadiliko katika chama.

Kwamba wanasiasa wanataaluma wa kila aina nao pia walijiunga na CHADEMA kipindi hicho. “Kuna kipindi tulikuwa tunajiita ‘Real Madrid’ maana tulikusanya ‘mastaa’ wote kutoka vyama vya upinzani.”

Freeman Mbowe aliifanya kazi hii ili kutoa fursa kwa Watanzania wengine kujenga chama imara cha siasa nchini ili si tu kuimarisha demokrasia nchini, bali pia kutoa mbadala kwa chama tawala na hata vyama vingine vya upinzani.

“Utekelezaji wa msingi huu wa chama umelipa. Haikuwa kazi rahisi, bali ni kazi makini yenye ujasiri wa kuepuka kujifanya Mbowe ndiye chama na badala yake kujenga chama taasisi ambapo wanachama wanaweza kusema demokrasia ndiyo CHADEMA.

Kwamba chini ya uongozi wake, Mbowe ameshirikiana na viongozi wenzake kupandisha chama kutoka chama cha tano mwaka 2000 mpaka chama cha pili mwaka 2010.

Zitto ni miongoni mwa vijana na Watanzania waliopata fursa ya kuchangia mabadiliko katika nchi kupitia juhudi hizi za Mbowe, hivyo kuifikisha CHADEMA hapa ilipo leo.

Anasema kuwa chama kilichojaa ufuasi wa watu kitapasuliwa na nyufa za uongo, fitna, chuki, majungu na kujipendekeza. Chama cha misingi ndiyo chama tunachopaswa kujenga na kujivunia nacho.

Ni ujasiri wa kufuata misingi ndiyo unaweza kumfanya kiongozi mwenye timu iliyojaa watu wenye vipawa mbalimbali na uwezo mkubwa wa kuvutia ‘wafuasi’ kama CHADEMA kumudu jahazi na kuliendesha vema.

Nimeanza kwa kumnukuu kaka na rafiki yangu Zitto ili kujenga msingi wa mada yangu leo.

Ninachojaribu kusema ni tofauti ya wanasiasa makini vijana ndani ya chama na wafuasi wanotaka kuonekana ili kukidhi maslahi.

Hoja ya Zitto iko wazi kuwa mafanikio ya kisiasa ni kujitoa kwa kila namna, waweza kudharaurika, kuzushiwa, kutuhumiwa na kutukanwa lakini kama unafanya jambo la msingi kwa manufaa ya wengi, utafanikiwa.

Kwa bahati mbaya, CHADEMA inakoelekea inaanza kuzingirwa na vijana wengi wasio na sifa za misingi alizozieleza ndugu yangu Zitto. Wengi wanaoingia huko wamekata tamaa na mfumo wa utawala wa CCM.

Vijana hawa wa kileo wanaingia CHADEMA kama tumaini, lakini bado wanahitaji kufundwa waijue misingi na maelngo ya chama kuwa si kuvalia ‘kombati’ kutoa matamko kila kukicha na kugombania vyeo na fedha.

Kasoro hii ndiyo imeanza kuwatafuna baadhi ya viongozi wa Baraza la Vijana Taifa la CHADEMA (BAVICHA), hivyo kukubali kutumika kama mawakala wa mafisadi kukihujumu chama chao kwa bei ndogo.

Laiti hawa wangekuwa na misingi anayoileza Zitto wangikuwa nawashinda kwenye mitandao ya kijamii wakijaribu kuandika taarifa za kuwakashifu viongozi wao wakuu kwa kutumia majina ya bandia, badala yake wangekuwa kama Mbunge wa Arusha Mmjini Godbless Lema.

Desemba 30 mwaka jana, niliandika makala yenye nikisema CHADEMA iwafunde BAVICHA mwaka 2013.

Nileleza kuwa mwaka 2012, ulikuwa na hekaheka nyingi kila nyanja lakini nikampongeza Godbless Lema, ambaye kwangu namwona kama mkomavu kisiasa.

Nikasema kuwa laiti CHADEMA ikipata vijana makini 20 kama Lema ikawasambaza mikoani kuwatia wananchi matumaini kuwa ukombozi mpya unawezekana bila kulaghaiwa kwa fedha na kurahisisha kazi ya kueleke Ikulu 2015.

Nilikumbusha jinsi Lema alivyovuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu lakini kwa takribani miezi tisa aliyokaa nje ya Bunge akisubiri uamuzi wa rufaa yake katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, alihangaika kukisambaza chama kwa umma.Darasa la Lema limetosha kuwafunda vijana wa CHADEMA kufuata misingi alioieleza Zitto, hivyo kujitathmini na kujipima kama wanaweza kasi ya chama hicho kuwa ni kuwatumikia wananchi bila kutanguliza ubinafsi.

Hizi kasoro tulizozisikia kwa BAVICHA kuwa wanatumiwa na mamluki kukisambaratisha CHADEMA, zinatokana na vijana husika kutokulia kwenye misingi ya uwazi. Hawa wametanguliza ubinafsi na tamaa ya mali na vyeo.

Kumbe iko kila sababu ya Mbowe kuendeleza darasa lake la misingi ya chama ili wafuasi wao wajue kuwa CHADEMA si kuvaa ‘kombati’ na kupayuka kwa kukinzana wenzako.

Anayefanya sarakasi za ajabu kama baadhi ya vijana hao wa BAVICHA waliotimuliwa uanachama, huyo atambue kuwa ndani ya CHADEMA kumbe anakuwa amepotea njia, bora akabaki CCM ili atumike vizuri kuvuruga vuguvugu la mabadiliko.

Wito wangu kwa vijana wapenda mabadiliko walioko ndani ya CHADEMA na vyama vingine, nawasihi watambue kuwa siasa ya leo ni ngumu hasa kwa yule anayeifanya bila kukubali kuwa kibaraka wa watafuta vyeo na madaraka. Tafakari

Tuesday, January 8, 2013

Mtuhumiwa kesi ya Dk. Ulimboka atoa siri nzito

• Azungumza na simu kwa kificho kutoka Gereza la Keko

SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Makao Makuu na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa kauli tata kuhusu uchunguzi wa tukio la kutekwa, kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, mtuhumiwa pekee katika kesi hiyo hadi sasa, raia wa Kenya, Joshua Mulundi, ameibuka na kutoa kauli na siri nzito ya tukio hilo.

Mtuhumiwa huyo ambaye yuko mahabusu, ameliambia gazeti hili kuwa anataka upelelezi wa kesi yake ukamilike haraka ili atendewe haki, lakini kubwa kuliko yote ameitaka serikali imlete Dk. Ulimboka mahakamani ili aweze kumtambua.

Akizungumza kwa kificho kwa njia ya simu kutoka ndani ya Gereza la Keko alikohifadhiwa, raia huyo wa Kenya alisema ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kusoma taarifa ya gazeti hili juzi ilikionesha polisi wakirushiana mpira na kutoa kauli zinazopingana kuhusu tukio la Dk. Ulimboka.

Alisema hadi sasa haoni maendeleo ya kesi hiyo kwani kila ikifika mahakamani, upande wa mashitaka hutoa hoja ya kutaka iahirishwe kwa madai kuwa upelelezi haujakamilika.

“Kila ninapoenda mahakamani naiomba mahakama imlete Dk. Ulimboka anitambue, nahoji kwanini upelelezi haujakamilika. Kwa bahati mbaya sana siku hizi kesi hii inapokuja mahakamani, hata vyombo vya habari havijulishwi. Nashukuru Mungu nimepata namba zenu za simu kutoka kwenye gazeti lenu ili nitoe ya moyoni...

“Naomba Dk. Ulimboka aletwe mahakamani ili anitambue, kama atasema mimi ndiye niliyemteka na kumtesa, basi kesi iendelee na sheria ichukue mkondo wake, kama atasema sikuhusika, basi kesi iishe maana sioni sababu ya mimi kuteseka hapa gerezani kwa kusubiri upelelezi ambao haujulikani utaisha mwaka gani,” alisema Mulundi.

Kwa mujibu wa mtuhumiwa huyo, amepata kutoa malalamiko kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akiiomba serikali imlete mbele yake, Dk. Ulimboka ili amtambue na kuhakikisha upelelezi wa kesi hiyo unafikia tamati.

Mbali ya maombi hayo, mtuhumiwa huyo wa kesi inayovuta hisia za wengi ndani na nje ya nchi, pia alisema aliwaomba viongozi hao wamsaidie kupata dhamana kwani kesi inayomkabili inaruhusu dhamana na hana wakili wa kumtetea.

“Dk. Nchimbi alipokuja hapa gerezani nilimwambia, lakini aliniangalia tu bila kujibu kitu. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Kairuki nimemwambia, DPP nimemwandikia barua na hata Balozi wa Kenya nchini Tanzania nimemwandikia, hajanijibu wala hakuna msaada ninaopata. Naomba serikali, jamii inisaidie kesi hii imalizeke haraka,” alisema mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alitoa siri nzito ya kile alichokieleza kuwa, ukweli kuhusu Dk. Ulimboka, jinsi alivyokamatwa, kuhojiwa na kufikishwa mahakamani katika mazingira aliyodai tatanishi, ambayo gazeti hili kwa sasa haliwezi kuripoti kwani kufanya hivyo ni kuingilia mwenendo wa kesi iliyopo mahakamani.

Wakati Dk. Ulimboka alitekwa Juni 26 mwaka jana na watu wasiojulikana, mtuhumiwa huyo alikamatwa Julai 3 na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kitusu, Dar es Salaam Julai 13.

Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari uliotikisa nchini katika nyakati tofauti mwaka jana, alitekwa, kuteswa, kupigwa hadi kung’olewa meno na kucha na kisha kutupwa katika msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alitangaza kuunda tume ya wataalam kutoka ndani ya jeshi hilo, iliyoongozwa na ACP Ahmed Msangi.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Dk. Ulimboka mwenyewe kuwataja baadhi ya watu aliodai kuwa ndio walihusika kumteka na kumtesa, lakini hadi sasa Mulundi, ndiye mtuhumiwa pekee aliyekamatwa.

Hata hivyo, tume hiyo haijawahi kutoa ripoti yake kama Kova alivyoahidi pamoja na kwamba hata majeruhi mwenyewe, Dk. Ulimboka hajawahi kuhojiwa, huku vigogo wa jeshi hilo wakitupiana mpira kuhusiana na sakata hilo.

Katika hatua ya kushangaza, juzi jeshi hilo kupitia kwa msemaji wake, Advera Senso, limekanusha kuwepo kwa tume hiyo likisema kuwa walioteuliwa ni polisi ambao watafanya kazi za kiuchunguzi kwa taratibu za polisi.

Kauli ya Senso ilipingana na ile ya Kova, ambaye juzi alikiri kuwepo kwa tume hiyo, lakini akasema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa vile taarifa zake alishazipeleka kwa wakubwa wake makao makuu baada ya kukamilisha wajibu wake.

“Hili suala lipo mahakamani kwanza, na kuhusu kuhojiwa au kutokuhojiwa kwa Dk. Ulimboka hilo lipo kwa mkubwa wangu, sasa unataka mimi niseme kama amehojiwa au la wakati sijui kinachoendelea huko?” alisema Kova.

Lakini Senso alisema kuwa, hakukuwepo na tume hiyo na kwamba walioteuliwa ni polisi ambao walifanya kazi za kiuchunguzi kwa taratibu za jeshi hilo.

Alisema Jeshi la Polisi lisingeweza kuunda tume katika suala la Dk. Ulimboka kwa kuwa kilichotokea ni uhalifu kama mwingine na litashughulikiwa kwa mujibu wa jeshi hilo.

“Kwanza hilo ni suala la mwaka jana na sisi ripoti za mwaka huo tumeshafunga, labda nianze kufuatilia sasa hivi kujua limefikia wapi,” alisema Senso.

Wakati vigogo hao wakisigana katika kulifafanua sakata hilo, Dk. Ulimboka mara kadhaa amekuwa akieleza kuwa yupo tayari kutoa maelezo yake kama kutakuwa na tume huru ambayo si hiyo iliyoundwa na polisi.

Katika tamko lake mwishoni mwa mwaka jana lililosomwa kwa niaba yake na wakili wa kujitegemea, Nanyoro Kicheere, akimwakilisha mwanasheria wake, Dk. Ulimboka alisema wapo watu ambao hawatapenda kusikia siri iliyojificha katika tukio zima la kutekwa kwake na kwamba hana jinsi zaidi ya kueleza ukweli.

Alisema kuwa tukio la kutekwa kwake, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno, na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande, lilitokea wakati akiwa kikao na ofisa aliyetambulishwa kwake ni ofisa wa Ikulu, Ramadhani Abeid Ighondu

Lema: Kiti cha Meya Arusha kinanuka damu

UMATI mkubwa wa wakazi wa Jiji la Arusha, jana walijitokeza kwenye Uwanja wa mpira wa Ngarenaro, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka miwili ya mauaji ya watu watatu waliouawa na polisi wakati wa maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Maandamano hayo yaliyofanyika Januari 5 mwaka 2011, yakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na wabunge kadhaa wa chama hicho, yalilenga kupinga uvunjwaji wa sheria, kanuni na taratibu zilizotumika kumweka madarakani Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo.

Wanaodaiwa kuuawa siku hiyo kwa kupigwa risasi na polisi wakiwa kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha ni Denis Shirima, Omary Ismail na raia wa Kenya, Paul Juguna.

Awali kabla ya mkutano huo wa jana kuanza majira ya saa nne asubuhi, viongozi wa CHADEMA wilaya na mkoa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema walitembelea vituo mbalimbali vya yatima na kutoa msaada wa mchele kilo 20 na mafuta ya kula lita tano kwa kila kituo.

Katibu wa CHADEMA wilayani hapa, Martin Sarungi alisema wamepanga kuendelea na kazi hiyo hadi Januari 21 ambapo kwa siku ya jana walifanikiwa kutembelea kituo cha Huruma Group kilichopo Kata ya Ngarenaro kinachohudumia waathirika wa virusi vya ukimwi, kituo cha watoto yatima cha Ansaar Muslim Youth Center kilichopo Kata ya Sombetini kinachohudumia watoto wa kike zaidi ya 30, kituo cha watoto yatima cha Kibowa kilichopo Kata ya Lemara na kile cha Karama kilichopo Kata ya Olorien.

Sarungi alisema kuwa katika kipindi hicho wanatarajia kutembelea jumla ya vituo vya watoto yatima 12, wafungwa na mahabusu kwenye gereza kuu la mkoa la Kisongo na wagonjwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa lengo la kuwasaidia, kuwafariji na kuwatia moyo.

Kwa upande wake diwani wa viti maalum, Viola Likindikikoki (CHADEMA) alisema kuwa yeye na madiwani wenzake wataendelea na msimamo wa kutomtambua meya kwani licha ya kuingia kwenye wadhifa huo kinyume na sheria, pia kiti anachokalia kinanuka damu ya wananchi watatu wa Jiji la Arusha waliouawa bila sababu.

Naye kiongozi wa madiwani wa CHADEMA kwenye Halmashauri ya Jiji la Arusha, Isaya Doita aliwataka wananchi wa jiji hilo kuhakikisha wanashiriki kwenye vikao vya shule wanazosoma watoto wao ili waweze kuzibana bodi za shule na walimu wakuu juu ya michango mbalimbali wanayokusanya, lakini haina tija.

Alisema kuwa walimu wakuu wamejikita kwenye kukusanya michango pekee na kusahau majukumu ya kufundisha jambo linalothibitishwa na matokeo mabaya ya matokeo ya mitihani ya taifa ya darasa la saba na yale ya kidato cha pili ambapo amewataka wazazi kuwa wakali kuhoji fedha wanazochanga zinafanya nini kwani hazisaidii kuboresha taaluma kwenye shule hizo.

Doita ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ngarenaro alitaka wananchi wanaofanya biashara chini ya miti wasitozwe ushuru kwani hawapati huduma yoyote kwenye maeneo hayo, hivyo hakuna sababu za msingi za kuwatoza kodi.

“Ebu tumchokoze Mungu kwa kutoa sadaka kwa yatima na wajane ili Mungu aamue kama Gaudensi anatakiwa kuendelea kukaa pale au hastahili, tunafanya jambo hili kwa uoga kwani ni gumu mno mpaka naomba Mungu amrudishie akili aweze kutubu na kugundua aliingia kwa hila ili baraka hizi tunazompa zisigeuke laana kwake,” alisema.

Alisema hata kama leo wakikubaliana na Lyimo kukaa madarakani, haimaanishi kuwa itabadili mfumo wa wananchi wa Arusha kuhudumiwa na serikali yao, bali itaendelea kujenga mfumo mbovu wa kuchakachua haki na sheria nchini kwani ni haki kwa serikali kuhudumia wananchi wake, hivyo haki hiyo wataendelea kuipata wakati wakiendelea kupinga uovu wa uvunjifu wa sheria za nchi bila aibu.

Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Amani Golugwa alisema inasikitisha polisi kuua raia wasio na hatia ambao hata hawakuwa kwenye maandamano ya CHADEMA, huku ikiwaacha wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu na kutolea mafano wa raia wa Kenya, Njuguna ambaye anadaiwa kuuawa muda mfupi baada ya kushuka kwenye basi.

“Baada ya kumuua, walimchukua wakampeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mount Meru na kumbandika jina Chacha Mwita, lakini mimi na Lema tulipokwenda kuikagua maiti hiyo tulimkuta na kitambulisho kinachoonesha kuwa ni Paul Juguna kutoka Kajiado nchini Kenya,” alisema.

Naye katibu wa CHADEMA wilayani Arusha, Sarungi alisema kuwa wameanza maandalizi ya kupata ushindi kwenye chaguzi mbalimbali zijazo kwa kuanza kuorodhesha majina ya wanachama wake kwenye maeneo ya Jiji la Arusha.

Kwa upande wake, Mbunge Lema amesema kuwa hayuko tayari kuona Meya Lyimo akiongoza kikao wakati kuna watu walikufa, kuna yatima wameachwa, kuna wajane wameachwa kutokana na maandamano ya kumpinga.

“Tukiacha hili lipite wanaweza kufikia hatua ya kunyang’anya wananchi mali zao. Msivunjike moyo katika harakati za kupigania haki kwani hata Nelson Mandela alivumilia kukaa jela, leo tunaona Afrika Kusini iko huru basi na nyie msikate tamaa ili haki iweze kutendeka ndani ya taifa hili,” alisema Lema.

Alisema kuwa kuanzia sasa atahakikisha hakuna kikao cha baraza la madiwani wa jiji kinaitishwa bila wananchi kutangaziwa kama sheria inavyotaka ili waweze kuhudhuria kusikia kile kinachojadiliwa kwa mustakabali wa maendeleo ya jiji la Arusha jambo lililoamsha shangwe kwa wananchi hao

BAVICHA yaanika hujuma za CCM


BAADHI ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na viongozi waandamizi wawili wa CHADEMA wamedaiwa kufadhili vijana wa BAVICHA kuhujumu chama hicho.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana La CHADEMA (BAVICHA), John Heche, wakati akizungumza na waandishi wa habari kueleza sababu za kuwavua uongozi baadhi ya wanachama wao na kusimamishwa wengine kutokana na usaliti.

Heche, hata hivyo, hakuwataja kwa majina viongozi hao wa CHADEMA akisema kuwa wako nje ya mamlaka ya baraza analoliongoza, ingawa vyanzo vyetu vya ndani vilibaini kuwa ushahidi wa moja kwa moja ulimtaja Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda.

Kwa upande wa viogogo wa CCM, Heche alimhusisha moja kwa moja Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, kuwa nyuma ya watu waliokuwa wakikichafua chama.

Alisema mwaka jana Wasira alikuwa akitoa kauli ya mara kwa mara kuwa mwaka 2013 CHADEMA itakufa kwa kuwa alikuwa anajua kuna watu atawatumia ndani ya CHADEMA kwa ajili ya kutaka kujaribu kufanikisha kauli yake hiyo.

“Sisi tulijiuliza huyu anapata wapi ujasiri wa kusema CHADEMA itakufa wakati ndiyo kwanza inazidi kunawiri? Tukajua mwenye uwezo wa kujua hiki chama kitakufa lini ni mwenyezi Mungu.

“Kumbe mwenzetu alikuwa na watu wake ndani ya chama waliomhakikishia kifo hicho, sasa tumewatimua akaanze upya,” alisema.

Heche alifafanua kuwa hivi karibuni kamati ya utendaji ya BAVICHA ikikutana jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi na uhai wa baraza nchi nzima kutoka mikoa yote ya kichama.

Aliongeza kuwa miongoni mwa maazimio ya kamati hiyo yalikuwa ni kupokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo ya BAVICHA iliyopewa kazi ya kuchunguza tuhuma za baadhi ya viongozi na wanachama wake.

Baada ya kupokea taarifa hiyo walibaini kuwa baadhi ya viongozi na wanachama wana hatia na kuwachukulia hatua zilizostahili kwa mujibu wa katiba ya BAVICHA.

Alimtaja kiongozi aliyevuliwa madaraka na ambaye pia atakuwa amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa CHADEMA kuwa ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wao, Juliana Shonza, huku wanachama wa kawaida waliovuliwa uanachama wa BAVICHA wakiwa Habib Mchange na Mtella Mwampamba.

Wanachama waliopewa onyo ni Gwakisa Mwakasando, Joseph Kasambala ambaye ni mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Mbeya pamoja na Ben Saanane.

Hata hivyo, Wilson Makala wa Babati, hakuwa miongoni mwa wanachama waliosimamishwa kwa muda kama ilivyoripotiwa kimakosa na gazeti hili.

Heche alisema Shonza katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti, alikuwa akishirikiana na baadhi ya watu kupanga njama na kufanya usaliti dhidi ya BAVICHA, chama na vijana wenzake wapenda mabadiliko.

Alisema katika mikutano hiyo ya siri kwa manufaa ya CCM, Shonza alikuwa akiwakusanya vijana wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliosimamishwa masomo au kufukuzwa vyuoni ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wanachadema wa Vyuo Vikuu (CHASO) na kuwarubuni.

“Juliana alifanya kazi yake hiyo kwa ushawishi wa hongo, ili wakubali kuitisha mikutano na waandishi wa habari, watoe matamko machafu dhidi ya CHADEMA na viongozi wake wakuu, akiwamo Dk. Willibrod Slaa na Freeman Mbowe,” alisema.

Alitaja moja ya mikutano hiyo kuwa ni ile iliyofanyika katika Bar ya Highland Makumbusho na kuwaita viongozi wa CHASO na kuwashawishi kuwa watakuwa na maisha mazuri, watarudishwa vyuoni na kutunzwa vizuri hapa mjini kama anavyoishi yeye endapo wangelikubali kufanya kazi hiyo.

Heche aliongeza kuwa Juliana alishiriki kikao kingine kwa ajili ya kuihujumu CHADEMA cha Desemba 6 mwaka jana katika Hoteli ya MIC kuanzia saa 12 jioni akiwa na baadhi ya wasaliti wengine.

Pia alisema Juliana alikaa na kushiriki vikao vya kuanzisha chama kipya kinachoitwa Chaumma, kushiriki katika makundi yaitwayo Masalia na PM7 ambayo yote yalikuwa na lengo la kuvuruga chama na kuwakosanisha wanachama.

“Kama tutashindwa kuwajibishana wenyewe kwa wenyewe katika makosa yenye ushahidi kama huu basi tutakuwa hatuna sababu ya kupewa nchi mwaka 2015 kwa kuwa hawa wasaliti hawawaathiri Wanachadema tu bali kila Mtanzania mpenda mabadiliko,” alisema