Kwanza kabisa ni vema ikaeleweka kwamba mradi ambao wawekezaji kutoka China na Oman walikuwa tayari kuutekeleza unajulikana kama Bagamoyo Special Economic Zone- kwa kiswahili - Eneo la Ukanda Maalum wa Uchumi Bagamoyo. Ujenzi wa Bandari- ni moja ya component Nne za Mradi huo mkubwa. Component nyingine za mradi ni ujenzi wa eneo la viwanda (industrial park) ambalo katika awamu ya kwanza litakuwa na viwanda 190 vitakavyozalisha ajira mpya za moja kwa moja 20,000 na awamu ya pili na tatu ikikamilika kutakuwa na viwanda 790- zitakazozalisha ajira mpya 100,000.
Component ya tatu ni ujenzi wa mji wa kasisasa wa makazi unaonendana na mahitaji ya karne ya 21. Ujenzi wa mji huu utasaidia kupunguza msongamano wa jiji la Dar es saalaam kwani shughuli nyingi za uchumi zitakazotokana na Bagamoyo Speciam Economic Zone zitapelekea watu wengi kuhamia kutoka Dar es salaam kwenye mji mpya.
Component ya nne ni logistics Park ambayo itafanya bagamoyo kuwa kitovu cha usaifirishaji wa mizigo na hivyo kuimarisha Tanzania kama transit route ya mizigo inayotoka na kuingia kwenda sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi- hii logistic park ndio ita handle transshipment kutoka Afrika kwenda Ulaya na Marekani
Concept ya mradi huo imefanana na concept ya mradi wa Shenzen- Special Economic Zone ambayo Kampuni inayotaka kuwekeza Bagamoyo ilikuwa mojawapo ya kampuni zilizowekeza
Bahati mbaya watu wengi wanajikita kuzungumzia bandari na huenda hata maamuzi ya kuukata mradi yamefanyika kwa kuzingatia component moja tu ya bandari na wameacha kufikiria manufaa makubwa ya ajira hasa kipindi hiki ambacho vijana wengi wa Tanzania wanamaliza shule bila matumaini ya kuajiriwa.
Mradi huo mkubwa umekuwa gumzo sehemu mbalimbali ulimwenguni kutokana na ukubwa wake pamoja na athari zake kwa maslahi ya makundi mbalimbali ulimwenguni.
Kwa mataifa ya Magharibi mradi huo ulikuwa tishio kwa consideration za ushindani na ushawishi ndani ya ukanda wa bahari ya Hindi ambao unabashiriwa kuwa kitovu muhimu katika bishara ya kimataifa katika miaka michache ijayo. Wazungu waliuona mradi huo utaipa China nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi.
Kwa mataifa mengine kama Afrika ya Kusini - mradi huo ulikuwa tishio kwa maslahi yao ya kiuchumi kwakuwa ungepelekea ushindani mkubwa kwa Biashara ya Bandari ya Durban ambao hivi sasa ndio kuna bandari pekee zenye uwezo wa kuhandle 4th generation ships.
Kwa Kenya, mradi wa Bagamoyo ulikuwa ni tishio kubwa kwa mradi wa Bandari mpya wanayopanga kuijenga huko LAMU ambayo itakuwa na uwezo wa kuhandle 4th generation ships na pia itakuwa na kitovu cha usafirishaji wa mafuta barani Afrika
Benki ya Dunia - nayo imekuwa negative juu ya mradi huo - na imetumia influence yake kwa Serikali kutokana na misaada na mikopo ambayo inaipatia Tanzania, kupenyeza ushawishi wa kuupinga mradi. Inafahamika Benki ya Dunia ni chombo kinachotumika na mataifa ya magharibi kutingisha serikali za Afrika pale zinapokiuka interest za wakubwa. Tumeona jinsi walivyoibana serikali kutizama
Upya baaadhi ya sheria zake mpya ili iweze kutoa ahadi za mikopo. Hoja waliyotoka nayo kupinga mradi wa Bagamoyo ni kwamba - kwakuwa wao wameipa Serikali mkopo wa maboresho ya bandari ya Dar es salaaam- endapo mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone utatekelezwa, utaleta ushindani kwa Bandari ya Dar es salaam na hivyo kushindwa kulipa mkopo.
Makundi haya matatu yalikuwa na common interest ya kuhakikisha kwamba Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone hautekelezwi. Imetumika nguvu kubwa ya ushawishi kwa kutumia propaganda za vyombo vya habari; economic intelligence; political influence & scare mongering techniques kuhakikisha mradi huu hausimami. Kazi waliyoifanya kwa mafanikio makubwa.
Ni vizuri kuzichambua hoja zinazotolewa dhidi ya mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone ili kuona kama kuna mantiki.
Hofu ya Serikali kupoteza mapato kutokana na ushindani wa Bandari ya Bagamoyo
Ukiangalia kwa juu juu hoja hiyo ina mantiki. Kwamba kutakuwa na ushindani na Dar es salaam itapoteza mapato. Lakini yapo mambo matatu yanayothibitisha kwamba hoja hiyo sio sahihi.
1) Bandari ya Bagamoyo itahudumua meli kubwa (4th generation ships) ambazo hivi sasa haziwezi kuingia katika bandari ya Dar es salaam. Katika biashara ya kimataifa hivi sasa, usafirishaji kwa kutumia meli kubwa ndio wenye tija, unafuu na faida. Kwa mfano leo hii kusafirisha bidhaa X kutoka Tanzania hadi China au Marekani kwa kutumia meli ndogo inagharimu mara mbili ya gharama ya usafirishaji kwa meli kubwa. Kutokuwa na uwezo wa ku handle meli kubwa kumefanya gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka Nchi zetu kwenda kwenye masoko kuwa kubwa (uncompetitive). Ndio maana leo hii nchi za Latin America ambazo zipo mbali kabisa na China, zinauza bidhaa zake nyingi katika soko la China kuliko nchi za Afrika ambazo zipo karibu na China kijiografia. Mfano halisi umetokea majuzi- Marekani ilipoanza vita ya biashara na China kwa kuongeza kodi katika bidhaa za China, in response China waliongeza kodi kwa maharage ya soya kutoka Marekani. Ikumbukwe kwamba biashara ya soya ni kubwa sana kwa Marekani- kila mwaka wanauza soya ya thamani ya Usd 35 Billion na zaidi kwa China. Hivyo kitendo cha China kuongeza kodi, gharama za soya zikapanda na hivyo wanunuzi wa soya kutoka China walitafuta altenative source ya soya- badala ya kuja Afrika, walikwenda Latin Amerika- moja ya sababu ya kwenda kule pamoja na mambo mengine ni uwepo wa bandari zenye uwezo wa kuhandle meli kubwa ambazo ni nafuu katika usafirishaji. Afrika imekosa fursa ya biashara kubwa sababu hiyo.
2) Uwepo wa bandari kubwa katika eneo moja huongeza wingi wa shughuli za usafirishaji wa mzigo kutoka kwenye bandari kubwa kwenda kwenye bandari ndogo. Mzigo mkubwa ambao ungeshushwa Bagamoyo ungetengeneza fursa ya biashara kwa meli ndogo na za kati kuuchukua Bagamoyo na kuupeleka kwenye bandari za jirani za Dar, Tanga, Mombassa, Beira nk
3) Ni vizuri pia kujiuliza hicho tunachoki protect (Katika Bandari ya Dar) manufaa yake ni zaidi ya manufaa tutakayopata katika Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone? Hivi sasa hivi Bandari ya Dar es salaam inaajiri watu wangapi? Baada ya upanuzi utakaofanywa ajira ngapi zitaongezeka? Ukweli ni kwamba kwa teknolojia za karne ya 21 shughuli za bandari zipo digitalized sana kiasi kwamba ile asili ya kuzalisha ajira nyingi haipo tena. Hivyo kwa vyovyote vile ajira mpya zitakazozalishwa baada ya kumalizika upanuzi hazitozidi 1000. Kwa upande mwingine, ajira zitakazozalishwa kwenye mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone- katika awamu ya kwanza tu ni 20,000. Je faida ipi wapi?
Kwa upande wa mapato (direct income) kwa Bandari ya Dar es salaam- serikali inapata kiasi gani? Kwa vyovyote vile mapato ya jumla ambayo serikali itakayapata katika mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone yatakuwa ni makubwa zaidi- kwani mbali na mapato itakayopata katika component ya bandari kwa njia ya Whaphage charges; import duties kwa bidhaa nyingi zitakazopitia katika bandari hiyo- serikali itapata kodi za aina mbalimbali katika viwanda 190 na baadyad 790 vitakavyojengwa. Watumishi 20,000 tu pay as you earn yao itakuwa ni kiasi kikubwa cha uhakika kwa serikali. Achilia mbali multiplier effects zitokanazo na shughuli za viwanda. Katika mji mpya utakaojengwa Serikali itapata kodi za majengo na kodi nyingine zitokanazo na ardhi na pango... achilia mbali kodi za shughuli nyingine za biashara zitakazofanyika Bagamoyo.
Hoja nyingine inayotolewa ni kwamba kumpa mgeni aendeshe bandari ni hatari kwa usalama wa nchi. Hapa cha kujiuliza- ndani ya Bandari ya Dar es salaam kuna kampuni ya Nje TICTS imeendesha shughuli zake ndani ya bandari kwa miaka 20 na zaidi - ni usalama upi umeathirika?
Inapokuja kwa hoja za kiusalama, China inamahusiano ya karibu sana ya kijeshi na Tanzania. Kila leo tumeona vikifunguliwa vyuo, viwanja vya ndege nk kwa msaada wa China. Wanajeshi wengi wa Tanzania wamepata mafunzo China na vifaa vingi vya kivita vimetoka China. Ni jambo la kawaida kukuta gari yenye number za JWTz ndani yake kuna askari wa Tanzania na China... sasa kwa ukaribu huo wa kihistoria tangu JWTZ ilipoanzishwa baada ya kuvunja jeshi lenye asili ya kikoloni lililojaribu kufanya mapinduzi miaka ya 60, leo hii sisi ndio watu wa kuhofia usalama dhidi ya Wachina?
Hoja nyingine inayozungushwa ni kwamba eti Wachina watanya'ngyanya mali za taifa endapo mradi huo utapata hasara kama ilivyokuwa kwa mradi wa Bandari wa Sri Lanka. Ukweli ni kwamba mradi wa Bagamoyo sio sawa na mradi wa Sri Lanka au mradi wa ujenzi wa Reli ya Kenya. Tofauti na miradi hiyo miwili ya Kenya na Sri Lanka, mradi wa Bagamoyo unatekelezwa kwa njia ya uwekezaji kwa asilimia 100- wakati ile miradi ya Kenya na Sri Lanka inatekelezwa kwa mikopo ambayo nchi inawajibu wa kuweka dhamana (sovereign guarantee). Maana yake nini? Hata kama mradi wa Bagamoyo utapata hasara, atakayeumia ni mwekezaji na sio Serikali. Lakini kwa uzoefu wa kampuni ya China Merchant katika uwekezaji wa miradi mikubwa ya aina hii, haiwezekani wakafanya uamuzi wa kuwekeza mradi wa kupata hasara kirahisi namna hiyo. Ikumbukwe kwamba kampuni ya China Merchant ina uwezo wake kimtaji unaofikia mara 20 ya GDP ya Tanzania.
Hoja nyingine inayosemwa eti masharti ya kuendesha mradi wa bagamoyo ni magumu. Hivi mahala ambapo watu wanazungumza- kila upande una wajibu wa kuja na mapendekezo yake (proposal) na upande wa pili una haki ya kuja na counterproposal. Kuweka mpira kwapani sio njia sahihi. Kama serikali iliweza kwenda extra mile kuvutia mradi wa Bomba la Mafuta la Uganda kwa kutoa vivutio maalum vilivyopelekea hadi kufanyika mabadiliko ya sheria Bungeni- under miscleneous ammendment? iweje ishindwe kufanya hivyo kwa Mradi wa Bagamoyo? Kwa faida za ajira na kodi zinazokuja na mradi wa Bagamoyo kwa hakika zinazidi faida za mradi wa bomba la mafuta ambalo sehemu kubwa ya ajira zake zitatokea wakati wa ujenzi wa bomba lenyewe na likishakamilika ajira zitapungua kwa asilimia 80.
Ukiachilia faida za moja kwa moja zilizotajwa kuhusu mradi wa Bagamoyo, ni wazi kwamba ujenzi wa mradi huo pia utasaidia kuufanya mradi wa reli ya Kati ya Standard Gauge kupata idadi kubwa ya mizigo ya kusafirisha ili uweze kurejesha mikopo iliyochukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo.
Kwa ujumla na vyovyote iwavyo, faida za mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone ni kubwa kuliko madhara tunayodhani tunayaepuka