Dk. Mgimwa: Sheria ya kodi iangaliwe upya
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, amesema ipo haja kwa serikali kuangalia upya namna kuboresha sheria ya kodi nchini, ikiwa ni pamojana kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija.
Dk. Mgimwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema bado kuna tatizo katika mfumo wa kodi, na kwamba serikali imejipanga kuboresha sheria hiyo ili ilete tija na maendeleo kwa Taifa.
“Serikali imekuwa ikipokea malalamiko kuhusiana na kuwepo kwa misamaha ya kodi na mfumo mbaya wa kodi kutoka kwa walipa kodi, serikali inakiri kuwepo kwa tatizo hilo na imejipanga kuboresha sheria ya kodi ili ilete tija kwa taifa,” alisema.
Aidha, Dk. Mgimwa aliongeza kwamba pamoja na changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo, kiwango cha ukusanyaji wa kodi kimeongezeka.
Alisema jumla ya Sh. bilioni 754 zilikusanywa Septemba mwaka huu, na kwamba kiwango hicho ni cha juu zaidi ya makusanyo ya mwezi yaliyowahi kukusanywa katika kipindi kikingine chote.
Akifunga maadhimisho hayo, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alisema kuna haja ya kuangalia upya zera za kodi pamoja na mfumo wa kusimamia vyanzo mbalimbali vya mapato, ili kubaini njia zitakazoongeza mapato ya ndani.
No comments:
Post a Comment