MSICHANA ALIEIGIZA KWENYE AIFOLA AMSHTAKI LINEX KWA KUMPA KOFI LA UKWELI.
Msichana ajulikanae kama Janeth Bundala, ambae ameigiza katika video ya Aifola ya Linex, amemshtaki na kumchukulia Rb Linex kwa madai ya udhalilishaji kwa kumpiga kofi la ukweli ukweli wakati wakiigiza kwenye video hiyo. kwa mujibu wa Linex, Janeth alikua anadai kulipwa fidia ya shilingi millioni moja katika madai hayo, lakini Linex amemlipa shilingi laki tatu na kumalizana nae maana hakutaka mambo yawe makubwa. kama unakumbuka kofi hilo lilishaleta kelele wakati video hiyo inatoka na Linex aliomba msamaha kupitia vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya jamii. story hii imenishangaza kidogo yaani ni sawa na ukacheze mashindano ya ngumi halafu umshtaki mwenzio kakupiga lol.
No comments:
Post a Comment