Wednesday, October 3, 2012


Watani wa jadi wameshindwa kutambiana baada ya kutoka kwa sare ya 1-1 katika pambano la kusisimua uwanja wa Taifa. Simba walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu kwa bao la Amri Kiemba alieunganisha kazi nzuri ya Mwinyi Kazimoto wakati Yanga walisawazisha kipindi cha pili kwa mkwaju wa Penati uliofungwa kifundi na Said Bahanuzi baada ya beki Paul Ngalema kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Yanga walilazimika kucheza robo ya mwisho wakiwa pungufu baada ya Simon Msuva kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea ndivyo sivyo Juma Nyoso. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Yanga 1-1 Simba.

No comments:

Post a Comment