DHANA ya Muungano wa Tanzania
*Una nasaba moja
ZANZIBAR iko maili chache tu kutoka Tanzania bara. Kabla ya Muungano watu wake walikuwa wenye nasaba moja, sanjari na kutawaliwa na kutenganishwa na wakoloni wamekuwa na uhusiano wa karibu sana kwa karne nyingi hata kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo.Watanzania walioko visiwani wengi wao wana asilia ya bara.
Wana chembe za damu zisizo na tone la shaka. Kwamba wenyeji wa asili ya Zanzibar wengi wanatoka bara, Wahadimu na Watumbatu. Ukweli na uhakika unabainishwa na historia ya kuanzia biashara ya utumwa na kilimo cha karafuu. Ni dhahiri wengi wao wanatoka Tanzania bara.
Licha ya watu wachache huko visiwani kudai kuwa kuna watu pekee wenyeji wa asili ya Unguja, bila kueleza uasili wa hao unatokana na chanzo gani.
Mwingiliano wa tangu enzi za kale, unadhihirisha na kubainisha kuwa biashara haramu ya watumwa na kukua kwa zao la karafuu, kulichangia kuongeza mchanganyiko wa wenyeji wa Tanzania visiwani, walioanza kuweka maskani katika mji mkuu wa Ugunja.
Maelfu ya watu hao waliokamatwa katika maeneo mbalimbali kutoka bara walipelekwa Zanzibar kuuzwa kabla ya kusafirishwa kupelekwa Mauritius, Reunion, Arabuni na nchi nyingine kufanya kazi wakiwa watumwa.
Hata hivyo, kumbukumbu na historia inabainisha kuwa zao la karafuu lilichukuwa nafasi ya biashara ya utumwa baadhi ya watu waliokuwa wamekamatwa baadhi walibakia mjini Unguja na hatimaye kupelekwa mashambani kufanya kazi katika mashamba ya karafuu kutokana na kuwa tegemeo kubwa la uchumi wa Zanzibar.
Wakulima hao, kutoka Tanganyika na sehemu nyingine za mbali kama Malawi, Msumbiji walikuwa wakienda Zanzibar kwa wingi kufuata ajira ya vibarua wa kuchuma karafuu wakati wa msimu wa zao hilo. Mbali na kushiriki kulima, kupanda miche ya mikarafuu hadi miaka ya 1950.
Ujio wa wakoloni wa kiarabu na Waingereza haukuondoa mizizi ya uhusiano wa damu na undugu wa karibu. Licha ya kupandikiza chuki, (damu nzito kuliko maji) uhasama na matabaka , yamkini waliacha chembe za ubaguzi baada ya uhuru wa visiwa hivyo. Sumu hii ya ubaguzi inazidiwa nguvu ya uasili na nasaba za Watanzania wa visiwani na bara na hivyo kukosa mashiko kwa Tanzania ya leo.
Kihistoria Unguja haiwezi kutenganishwa na maeneo ya upande wa Tanzania bara, Mzizima, Msasani, Bagamoyo, Mafia, Kilwa, Saadani na Pangani, kiasili, mila za kinasaba kutokana na chimbuko lake.
Hata ile miingiliano ya kigeni na tawala zake, kabila za watu wake haikuathiri miingiliano ya watu wa visiwani na bara. Kama vile rangi na kuingia kwa dini mbili za Uislamu na Ukristu huko Unguja, kulibakia, japo neno Unguja linatokana na neno lililotolewa, la “ungo kujaa”, yaani ungo uliojaa matunda na nafaka, ndilo asili yake.
Historia na kumbukumbu zilizopo zinaonyesha wazi kuwa ukoo wa Pazi Mwinyimkuu kutoka mwambao wa Bagamoyo, ulihamishia maskani yake kwenda Unguja Ukuu. Ukiwa huko ulipanuka kizazi chake, na kuenea ni wakina Pazi Magombele, Pazi Kilome, Magimba na Digogo. Bila kuathiri mila na desturi, jadi na mwiingiliano wa nasaba.
Uhusiano huu wa kihistoria una manufaa makubwa kwa Watanzania, ndani ya Muungano Wanzibari wamekuwa wakinufaika na mambo muhimu, makazi ya kudumu, biashara, kumiliki ardhi, kuishi kwa uhuru ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Harakati za Uhuru, waanzilishi wake ni watu wa pande mbili, waasisi wake Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume kwa pamoja walishughulikia mambo ya kijamii na kiutamaduni hadi kuanzisha harakati za kisiasa, kuanzia na Chama cha African Association ambacho kilianzishwa Tanganyika, kikiwa chama kinachoshughulikia mambo ya kijamii na utamaduni. Kilianzishwa na Waafrika wa Dar es Salaam, na kuendelea kusambaa nchi nzima, pia chama hicho kilifungua tawi lake Zanzibar mwaka 1934.
Vyama vya Afro Shiraz Party na TANU, ndivyo viliendesha harakati hadi Tanganyika na Zanzibar baadaye kushika dola na kufuatiwa na Muungano wa nchi mbili mwaka 1964. Haya ni baadhi ya maeneo muhimu yanayokumbusha uhusiano wa kihistoria wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa bahati mbaya baadhi ya watu wanasumbuliwa na kasumba hatarishi yenye kudai na kubagua watu kwa uasili, ukabila na dini zao na wanadiriki kutaka serikali ya mkataba ambayo ni sawa na kuuvunja Muungano, hawajali athari, faida na hasara.
Na ni bahati mbaya sana watu hao ni waathirika wa kasumba hatarishi ya ubaguzi, baadhi yao wanadiriki bila soni kudai eti watu wa bara hawatakiwa kuishi Zanzibar. Ni watu hao hao wana makazi ya kudumu, biashara na wana miliki ardhi upande wa bara.
Ukibahatika kuivinjari kwa mapana historia ya nchi hizi mbili, kwa shingo upande unalazimika kuziita bara na visiwani nchi mbili, ili kwenda sanjari na matakwa ya baadhi ya watu wachache, lakini kiasili Watanzania wa visiwani na bara ni ndugu waliotenganishwa na ujio wa wakoloni. Ni dhahiri hakuna sababu ya kuwa na shaka kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya watu wenye nasaba.

No comments:
Post a Comment