Monday, November 5, 2012

JK azindua mradi wa maji


RAIS Jakaya Kikwete, amezindua rasmi mradi wa uzalishaji maji katika mkoa wa Singida utakaogharimu kiasi cha sh bilioni 31.1.

Mradi huo unaotarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 109,523 mkoani hapa sawa na asilimia 100 ya wakazi wote, ulianzishwa Novemba 2, 2009 na unatarajiwa kumalizika mapema Desemba.

Akizungumza na wananchi mkoani hapa, Kikwete alisema kuwa mradi huo utaweza kutosheleza mahitaji ya maji kwa asilimia 100 na hivyo kumaliza tatizo hilo.

“Mimi napenda niwahakikishie kwamba huu mradi utakapokamilika kamwe hamtakuja kupata shida ya maji katika mkoa huu, maana katika mikoa yenye uhaba wa maji Singida ni kinara ila sasa mtabaki mnasimulia tu,’’ alisema.

Rais Kikwete alisema mradi huo umefadhiliwa na benki ya Kiarabu kwa maendeleo ya Afrika (Badea) kwa kisai cha sh bilioni 7.2 pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Taifa (OPEC) uliofadhili sh bilioni 7.4.

Alisema kuwa serikali ya Tanzania kupitia programu ya maendeleo ya sekta ya maji imefanikiwa kutoa kiasi cha sh bilioni 10.4 ili kufanikisha mradi huo.

Naye Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alisema kuwa mradi huo utaongeza uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita 3,885,000 kwa siku na kufikia lita 21,093,000 sawa na asilimia mia moja

No comments:

Post a Comment