Nchi Takatifu ( Holly Land)
Kabla hujawa kama ulivyo tunaambiwa alikuwepo Mungu tu au kwa jina unaloweza kumwita kwa mazoea yako. Mungu ndiye Baba wa wote, aliye juu ya yote, aliye katika yote, na ndani ya yote. Bila yeye hakuna kinachokuwa kama kilivyo. Imeandikwa alifinyanga udongo na kupuliza ndani yake roho wa uhai, kisha binadamu akawa nafsi hai. Mungu aliye roho anaingia katika nyumba aliyoifinyanga mwenyewe. Tukiondoa roho wa Mungu aletaye uhai ndani yako wewe ni nchi, wewe ni udongo. Kwa Mungu aliye mtakatifu sana kuamua kuacha utukufu wake na kujihengea nyumba ya udongo na kisha kukaa huko, wewe umefanyika nchi Takatifu ( Holly Land), give thanks to God. Mpe utukufu Mungu wewe ni wa kipekee you are gods na kati yenu hakuna aliye zaidi ya mwingine.
Acha kuheshimu au kuhangaika kutafuta nchi takatifu, wewe ndiye nchi takatifu. Acha kutafuta mahala patakatifu pa kuhiji wewe ndiye mahala penyewe alipopachagua Mungu.. hiji ndani yako na endelea kumtolea Mungu Dhabihu za shukrani. Utu wako ndiyo maskani yake Mungu ambayo yanapendeza kama nini? Je unayatamani makao ya Bwana? Ingia rohoni mwako kutana Naye maana imeandikwa je hamjui kwamba ninyi ni hekalu la roho mtakatifu. Mungu ni roho na ajili yake wewe upo na kwa njia yake ukafanyika kuwa kama ulivyo. Wewe ni maskani matakatifu ya Mungu mwenyewe. Acha kukimbiakimbia kumtafuta kule na kule, yeye yupo ndani ya nyumba udongo ambayo ni wewe hapo. Jifunze kumtafuta ndani yako, yupo na hayupo mbali.
Wewe ndiye Taifa takatifu la Mungu na maskani halisi ya Mungu. Wewe ndiye Mungu aliyevaa mwili unaokufa, mwili unaochakaa, na mwenye kusambaratika. Wewe ni taifa la Mungu, ndani yako ni makao halisi ya Mungu. Ukitambua hilo utaanza kuwa huru na mafundisho ya yuko kule Arusha, Abuja, Mwanza, Mwenge au popote, wewe ndiye maskani yake mtazame kisha anza kufurahi pamoja naye. Anakupenda. Acha kutafuta fedha nyingi kumwendea Jerusalem au Oman au popote, huko hayuko bali huyo unayemsafirisha na anayeusafirisha mwili wako mpaka huko ndiye. Yupo ndani yako. Wewe ni Taifa takatifu, tambua hivyo na shangilia wewe si mnyonge hivyo usiruhusu unyonge tena.
No comments:
Post a Comment