Search This Blog

Friday, April 26, 2019

RIPOTI YA CAG KUHUSU SARE ZA JESHI, UKURASA No 310

Ripoti ya CAG kuhusu sare za Jeshi ,Kurasa No. 310

Moja ya maelezo ya CAG.


" Kukosekana kwa nyaraka za kuthibitisha uletaji wa mzigo. Niliomba Hati ya kupokelea Shehena ya Mzigo Bandarini (Bill of Lading), Hati ya Madai kutoka kwa Mtengenezaji (Commercial Invoice), Hati ya Mzigo ulipotoka (Certificate of Origin), orodha za mali zilizopo kwenye meli (Packing List) na cheti cha ukaguzi wa bidhaa (Inspection Certificate) kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders kwa ajili ya kujiridhisha kama bidhaa husika zililetwa nchini. Hata hivyo, Mzabuni alishindwa kuwasilisha nyaraka hizo.

 Aidha, nilipitia Mfumo wa Forodha (TANCIS)
wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na kubaini kuwa hapakuwa na shehena yoyote kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders mwezi Novemba 2015. d) Vilevile, nilifanya mahojiano na Maofisa wa Bohari kuu ya Jeshi la Polisi na kubaini hakukuwa na Sare zozote zilizoletwa na Mzabuni Daisy General Traders mwezi Novemba 2015.  Hivyo, Serikali imepata hasara kubwa kwa kufanya malipo ya Sare za Polisi ambazo hazikuletwa na Mzabuni. Kuhusu suala hili, nashauri Mzabuni Daissy General Traders arejeshe kiasi alicholipwa kwa kutoleta Sare za Polisi na hatua stahiki za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa Maofisa wote wa Jeshi la Polisi kwa kuisababishia Serikali hasara. "

No comments:

Post a Comment