CHADEMA yamvaa Wassira
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wakazi wa Jimbo la Bunda kubadili mtazamo wao kwa kuwachagua viongozi wachapa kazi.Akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Bunda juzi katika mkutano wa hadhara mjini hapa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Taifa, Godbless Lema, alisema matatizo ya watu wa Bunda kamwe hayataisha kama hawatafanya uamuzi wa kuachana na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Stephen Wassira ambaye alidai kazi yake ni kulala tu bungeni.
Alieleza baadhi ya upungufu wa Wasira ni pamoja na uzee, hali inayomfanya kusinzia bungeni kutokana na kushindwa kustahimili hoja ngumu zinazoibuliwa na wabunge vijana, wasomi wanaotaka mabadiliko.
“Watu wa Bunda walifanya makosa kuwa na mbunge mchapa usingizi bungeni…msisubiri malaika awaondolee usingizi wenu, wapeni CHADEMA nafasi, ili kutafuta uhuru na haki mliyopoteza kwa muda mrefu,” alisema.
Kuhusu kero ya maji, Lema alidai licha ya fedha nyingi zinazotolewa na serikali kwa maendeleo ya maji mjini Bunda, bado Wassira ameshindwa kukidhi mahitaji ya maji.
“Maji yako umbali wa kilomita 12, lakini watu wa Bunda hawana maji kwa sababu ya ufisadi unaofanywa na viongozi wa serikali,” alisema Lema
No comments:
Post a Comment