Waasi wa Somalia wa Al Shabab washindwa kijeshi
13 Disemba, 2012 - Saa 06:39
Jeshi la AU nchini lililopo Somalia
Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, anasema kundi la wanamgambo wa Al Shabab limeshindwa kijeshi.
Bwana Mohamud ameiambia BBC kuwa serikali yake inawatuma wazee wa kimbari ili kuwashawishi vijana waliokuwa wamehadaiwa kujiunga na Al Shabab, kutupilia mbali alichosema ni maadili potovu na kusitisha ghasia.
Serikali ya Somalia imekuwa ikiimarisha utawala wake, na kudhibiti nchi hiyo ikisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika. Kabla ya sasa, Somalia ilikuwa haijawa na serikali rasmi kwa zaidi ya miaka 20.
Hassan Sheikh Mohamud alichukua hatamu za uongozi mwezi Septemba mwaka huu
No comments:
Post a Comment