Search This Blog

Sunday, January 20, 2013

CAG ataka ofisi yake iwe huru

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amependekeza kuwa ofisi yake iwe taasisi ya kujitegemea ili iwe huru kufanya kazi bila kuingiliwa na idara nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kutoa maoni ya ofisi yake katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema watumishi wa idara hiyo wanapendekeza ofisi yake iwe taasisi inayojitegemea.

Utouh, alisema kuwa idara hiyo inafaa kuwa kama ilivyoundwa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) au Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuweza kufanya kazi zao kwa uhuru huku wakiweza kuajiri.

Akitolea mfano, CAG alisema wakati mwingine huitaji kuajiri, lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa kuwa kuna taratibu zinazowahitaji kuandika barua kwanza serikalini.

Aidha, mwasisi wa kupigania uhuru nchini aliyewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini, George Kahama, naye alitoa maoni katika ofisi za tume hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kile alichokieleza.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alipoulizwa juu ya maoni yaliyowasilishwa na Kahama aligoma kuzungumza

No comments:

Post a Comment