Search This Blog

Friday, October 12, 2012

Manispaa Kinondoni yakubali agizo la diwani



MANISPAA ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imekubali kutekeleza wito wa Diwani wa Kata ya Saranga, Efraimu Kinyafu kwa kuagiza Kampuni ya ujenzi ya Casco Costruction Ltd kuanza ujenzi wa barabara moja katika kata hiyo.

Injinia wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Gerard Urio, amesema Kampuni ya Casco sasa itaanza ujenzi wa barabara ya Kimara hadi King’ong’o Oktoba 15.

Kauli hiyo imekuja baada ya diwani Kinyafu kutoa siku saba za utekelezwaji wa ujenzi wa barabara hiyo, kinyume chake angewahamasisha wakazi wa eneo hilo kuandamana hadi kwa Mkurugezi wa Manispaa hiyo kufikisha kilio chao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Urio alisema wakazi hao wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kuwa mchakato wa kuanza ujenzi huo ulikuwa haujakamilika, na kwamba utaanza hivi karibuni baada ya kukamilika utiaji saini mkataba kati mkandarasi na manispaa hiyo, uliofanyika Oktoba 8 mwaka huu.

Alisema barabara hiyo inatazamiwa kukamilika Machi 3, mwakani na ujenzi wake utagharimu sh milioni 281, kati ya hizo sh milioni 250 zikiwa ni msaada kutoka Japan.

Alipoulizwa juu ya jambo hilo, Kinyafu alisema hadi sasa hana taarifa na akasema ni aibu kwa manispaa hiyo kwa kuwa haijawahi kutekeleza miradi ya maendeleo ya kata hiyo bila wananchi kutumia nguvu ya maandamano

No comments:

Post a Comment