Search This Blog

Friday, October 5, 2012

Bawabu wa papa mahakamani kwa wizi


Aliyekuwa bawabu wa Papa Benedict amerejea mahakamani katika kile kinachotarajiwa kuwa siku muhimu kabisa ya kesi yake mjini Vatican kwa mashtaka ya wizi wa nyaraka muhimu za siri kutoka ofisi ya Papa.

Nyaraka hizo zimefichua tuhuma za rushwa na mgogoro wa madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.

Bawabu huyo Paolo Gabriele, anatarajiwa kutoa ushahidi hii leo ikiwa ni siku ya pili ya kesi hiyo.

Makao makuu ya kanisa hilo Vatican wanasema kuwa Gabriele tayari amekiri mashtaka akisema kuwa alitaka tu kuweka hadharani uovu na rushwa ndani ya kanisa hilo.

Bwana Gabriele anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka minne jela iwapo atapatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment