Ukatili kwa watoto wa kike bado.
NAIBU WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema asilimia 49 ya watoto wa kike wanafanyiwa ukatili nyumbani hivyo kuathiri maendeleo yao kwenye elimu.
Mwalimu alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni ya Shirika la Plan International ya ‘Mimi ni Msichana’ pamoja na kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.
Alisema kiwango hicho cha watoto wanaofanyiwa ukatili ni kikubwa, hivyo kunahitajika ushirikiano na wadau mbalimbali, ili kuukomesha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Plan International, David Muthungu, alisema katika kuadhimisha siku hiyo ni bora kutambua matatizo ya watoto wa kike likiwamo suala la mimba za utotoni ambalo limekuwa chanzo cha kukatishwa masom
No comments:
Post a Comment