PPF yasomesha yatima 1,095.
MFUKO wa Hifadhi za Jamii (PPF) umetumia zaidi ya sh milioni 561 kulipia ada na gharama za masomo ya elimu ya sekondari kwa watoto 1,095 ambao wazazi wao walifariki dunia wakiwa wanachama wa mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Willium Erio, alibainisha hayo juzi alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kwa wajumbe wa mkutano wa 22 unaoendelea mjini hapa.
Alisema fedha hizo zililipwa kwa mwaka 2011 ambapo alisema watoto wanaonufaika na fao hilo la elimu ni wale ambao wazazi wao walikuwa wanachama angalau kwa miaka mitatu.
Erio alisema PPF walianza kutoa fao hilo kuanzia mwaka 2003 kwa lengo la kuwawezesha watoto wa wanachama ambao wamefariki dunia kuweza kuendelea na masomo na kwamba kwa sasa wanaangalia uwezekano wa kuwasomesha mpaka kidato cha tano na sita kwa wale watakaokuwa wamefanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha nne.
Alisema mfuko huo umeendelea kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wanachama kupitia vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) vilivyopo katika maeneo ya kazi, ambapo mpaka kufikia Juni mwaka huu jumla ya sh bilioni 45.4 zimetolewa kwa SACCOS 36
No comments:
Post a Comment